Jul 16, 2011

DAR ES SALAAM

BAADA YA BARAZA LA HABARI KUTENGENEZA MISWADA MIWILI YENYE LENGO LA KUPIGANIA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI, WANAHABARI, WADAU NA WANANCHI KWAPAMOJA, WAMETAKIWA KUJITOKEZA KUPIGANIA MISWADA HIYO ILI IPITISHWE NA SERIKALI.

WITO HUO UMETOLEWA HII LEO NA MWANAHARAKATI KATIKA KUPIGANIA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI PROFESSA ISSA SHIVJI, WAKATI AKICHANGIA MADA KATIKA KITUO CHA TELEVISHEN STAR TV ILIYOHUSU UHARIRI NA UWAJIBIKAJI, BAADA YA KUPITISHWA KWA AZIMIO LA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI.

HATUA HIYO IMEKUJA BAADA YA MUDA MREFU SASA TANGU IBAINIKE KUA SHERIA NYINGI ZILIZOPO ZINAZOHUSU UHURU WA VYOMBO VYA HABARI ZIMEKUA HAZITOI UHURU VYOMBO HIVYO BADALA YAKE ZIMEKUA ZIKI-ILINDA SERIKALI.

MIONGONI MWA MISWADA ILIYOPITISHWA NIPAMOJA NA KUITAKA SERIKALKALI KUZIBADIRISHA SHERIA HIZO ILI ISIWEZE KUJILINDA, AMBAPO SUALA HILO SHEVJI AMESEMA SI LAKUWAACHIA WATU WACHACHE BALI NI LAJAMII KWA UJUMLA.

WAKATI HUO HUO SHEVJI AMEWATAKA WATU KUAMKA NA KUUKUBALI UHURU WALIOPEWA KIKATIBA, KUTOKUWA WAGUMU PINDI WANAPOTAKIWA NA WAANDISHGI WA HABARI KUTO TAARIFA ZINAZOWAHUSU.

AIDHA KWA UPANDE WAO WADAU MBALIMBALI WA HABARI WAMESEMA KUA IKO HAJA SASA YA KUONA SUALA LA UHURU WA UPASHANAJI WA HABARI LIKAANZA KUFUNDISHWA MASHULENI.

.


Jul 15, 2011

KUTOKA MJENGONI DODOMA ILIKUA HIVI

DODOMA

KAMATI YA NISHATI NA MADINI, HII LEO IMEITAKA SERIKALI YA JAMHURUI YA MUUNGANO WA TANZANA, KUTOA MAELEZO YATAKAYO JITOSHELEZA KUHUSIANA NA MAAMUZI YAKE YA UNUNUZI WA MTAMBO MKUBWA WA KUZALISHA UMEME ULIO NA GHARAMA, HALIYAKUA SERIKALI HAINA GESI YA KUTOSHA YA KUUENDESHEA MTAMBO HUO.

KAULI HIYO IMETOLEWA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI JANUARI MAKAMBA, WAKATI AKIWASILISHA TAARIFA YA MAKADIRIA NA MAPATO YA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI YA MWAKA 2011/2012.

HATUA HIYO IMEKUJA BAADA YA KAMATI YA NISHATI NA MADINI KUBAINI KUONGEZEKA KWA GHARAMA ZA UZALISHAJI WA UMEME KWA SERIKALI, HUKU TATIZO LA UPATIKANAJI WA UMEME KWA WANANCHI WAKE LIKIZIDI KUONGEZEKA.

AIDHA KAMATI HIYO IMEITAKA SERIKALI KUTAMBUA KUA, UPUNGU WA MVUA HAUWEZI KUA SABABU KUBWA YA TATIZO LA UPATIKANAJI WA UMEME, HALI YAKUA NCHI INAJITOSHELEZA KWA KUA NA VYANZO VINGI VYA KUZALISHA NISHATI YA UMEME.

PAMOJA NA HAYO, KAMATI HIYO IMEISHAURI SERIKALI KUONGEZA JUHUDI ZAKE KATIKA KUWEKEZA KWENYE VYANZO HIVYO MBADALA VYA KUZALISHA UMEME PAMOJA NA KUUJUMUISHA MPANGO WA DHARULA WA TAIFA WA UPATIKANAJI WA UMEME KATIKA MPANGO WA MIAKA MIRTANO ULIOPITISHWA NA SERIKALI.

JANUARI MAKAMBA AMEWASILISHA MAKADIRIA NA MAPATO YA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI YA MWAKA 2011/2012, YENYE ZAIDI YA SHILINGI BILONI 402 NA MILIONI 412, AMBAZO ZIMEPINGWA NA MWAKILISHI WA KAMBI YA UPINZANI JOHN MNYIKA, WAKIITAKA SERIKALI IPUNGUZE BAJETI HIYO KUTOKANA NA MATUMIZI MABAYA YA ANASA YANAYOFANYWA NA BAADHI YA WATUMISHI WA WIZARA HIYO, HUKU WAKIWAACHA WACHIMBAJI WADOGOWADOGO MIGODINI WAKIFA NJAA

Jul 14, 2011

YEEEEEE MFAUME PASTORY NA ISSA NDOKEJI JOMBAAAAA KUTOKA CHUCHU FM RADIO





DODOMA

WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROF. PETER M. MSOLLA, HII LEO AMEWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2010/2011 YENYE ZAIDI YA SHILINGI BILIONI SITINI NA NNE MILIONI MIAMOJA KUMI NA SABA NA LAKI TANO SITININA MBILI ELFU.

KWA MUJIBU WA WAZIRI MSOLLA, MAMBO AMBAYO AMESEMA YATAPEWA KIPAUMBELE KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI HIYO, NI PAMOJA NA KUMALIZIA UKARABATI WA MAJENGO YA VYUO VYA SAYANSI NA TEKNOLOJIA HAPA NCHINI ILI KUSAIDIA KUONGEZA IDADI YA WATAALAM KATIKA SEKTA HIYO.

PIA SERIKALI IMEPANGA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA SUALA LA UTAFIKTI KUTOKANA NA NCHI KUWA NYUMA KATIKA SUALA HILO, AMBAPO HATUA AMESEMA MPAKA SASA HATUA KADHAA ZIMEKWISHA ANZA KUTEKELEZWA.

AIDHA AMEIAMBIA SERIKALI KUA WIZARA YAKE INAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA YA UKOSEFU WA RASILIMALI WATU, AMBAPO WIZARA YAKE KWA KUSHIRIKIANA NA TUME AMESEMA IMEJIWEKEA MKAKATI WA KUHAKIKISHA WANAHAMASIHA WATU KUSOMA MASOMO YA SAYANSI ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIYO.

LICHA YA CHANGAMOTO HIZO WAZIRI MSOLLA AMESEMA SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO ILI KUBORESHA HUDUMA ZA MAWASILIANO, AMBAPO AMETHIBITISHA KUA ZANZIBAR ITAUNGANISHWA KWENYE MKONGO HUO MARA BAADA YA KUKAMILIKA.

WILAYA YA MJINI UNGUJA

KITUO CHA KUWAENDELEZA VIJANA KIELIMU NA KITAALUMA(STON TOWN YOUTH CENTER), KIMEKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIREJA NYUMA MAENDELEO YA KIYUO HICHO.

HAYO YAMEELEZWA NA MRATIBU WA MRADI WA VIJANA ,JACKSON OGOTU WAKATI AKIZUNGUMZA NA CHUCHU FM OFISINI KWAKE KIKWAJUNI WILAYA YA MJINI ZANZIBAR.

JACKSON AMESEMA KITUO HICHO HUTOWA ELIMU TOFAUTI KWA VIJANA WA RIKA ZOTE, INGAWA KITUO HICHO KUWA NA WAFADHILI LAKINI KINAKABILIWA NA MATATIZO MBALIMBALI ,IKIWEMO UHABA WA FEDHA KWA AJILI YA KUENDELEZA MIPANGO WALIYOYAKUSUDIA.

AIDHA JACKSON AMEFAHAMISHA KUWA KITUO HICHO KIMEJIWEKEA MALENGO TOFAUTI KAMA KUWAKWAMUA VIJANA KIELIMU NA KITAALUMA NA, ILI KUWEZA KUFAIDIKA NA KUONDOKANA NA HALI NGUMU YA KIMAISHA.

SAMBAMBA NA HAYO AMEWATAKA VIJANA KWENDA KUJIUNGA NA KITUO HICHO NA KUACHA TABIA YA KUKAA MASKANI NA KUFANYA MAMBO YASIYOFAA KWA JAMII.


Jul 13, 2011

ROSTAM AZIZI MBUNGE WA IGUNGA AJIVUA GAMBA


Taarifa zilizotufikia kutoka Igunga Tabora kupitia kutuo cha Televisheni cha ITV zinasema Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa NEC wa chama cha mapinduzi CCM Rostam Azizi, amejiouzulu nyazifa zake hizo ambazo alikuwa nazo katika Chama cha mapinduzi CCM ambapo kwa sasa anaongea na wananchi wa jimbo hilo .

Mtangazaji wa ITV Samweli Kabendera ameripoti moja kwa moja kutoka Tabora akielezea juu ya tukio hilo, ambalo limetokea muda mfupi uliopita, gazeti moja liliripoti leo kuwa kipindi cha miezi mitatu kilichotangazwa na CCM kwa wanachama wake na viongozi kujivua gamba tayari kimefikia ukomo Hivyo tukio hili inawezekana ndiyo mwendelezo wa CCM kuchukua hatua za kujivua gamba ili kurejesha imani kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.

FAHAMU HILO KUTOKA BUNGENI NA ZANZIBAR

WILAYA YA KUSINI UNGUJA

MKUU WA WILAYA YA KUSINI UNGUJA HAJI MAKUNGU MGONGO AMEWAAHIDI WAKULIMA WA KIJIJI CHA MTENDE NA KIZIMKAZI DIMBANI KUA, ATASHIRIKIANA NA WIZARA YA KILIMO NA MALI ASILI, ILI KUHAKIKISHA WAKULIMA WANAPATA DAWA ZA KUUWA WADUDU WAHARIBIFU.

AMEYASEMA WAKATI AKIWA KATIKA ZIARA YAKE UZINDUZI WA KILIMO CHA MOGOMBA NA UVUNAJI WA MPUNGA KATIKA KIJIJI CHA KIZIMKAZI NA MTENDE WILAYA YA KUSINI UNGUJA.

AIDHA HAJI AMEWAPONGEZA WAKULIMA HAO KWA JITIHADA ZAO WALIZOZIFANYA KATIKA KUFANIKISHA KILIMO CHA MPUNGA NA KUAHIDI KUWA, ATAFANYA JITIHADA ZA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA KILIMO KUHAKIKISHA WANAPATIWA DAWA ZA WADUDU WAHARIBIFU ILI KUNUFAIKA NA KILIMO.

KWA UPANDE WAO WAKULIMA, WAMESEMA PAMOJA NA JITIHADA ZOA ZOTE ILA BADO WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO NYINGI AMBAZO ZINAHIJI KUPATIWA UFUMBUZI, ILI NAOWAWEZE KUFIKIA MALENGO WALIYOYAKUSUDIA.

PAMOJA NA HAYO WAMEIOMBA WIZARA YA KILIMO KUWA KARIBU NAO, ILI KUWEZA KUJUA MATATIZO YANAYO WAKABILI KATIKA KUENDELEZA KILIMO KWA LENGO LA KUNUFAIKA NA UKULIMA WAO.

DODOMA

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LAKUJENGA TAIFA DAKTARI HUSEEN ALLY MWINYI, HII LEO AMEWASILISHA BUNGENI BAJETI YA MAKADIRIO YA MATUMIZI NA MAPATO YA WIZARA YAKE, INAYOTARAJIWA KUTUMIA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MIASITA THEMANINI NA MBILI, BILIONI MIATATU THEMANINI NA TANO NA MIAMOJA ARUBAINI NA TANO ELFU KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012.

AKIBAINISHA MAMBO YALIYOPEWA KIPAUMBELE KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI HIYO, DK: HUSSEN AMESEMA WIZARA YAKE IMEPANGA KUAJIRI WANAJESHI WAPYA NA KUIMARISHA MAFUNZO YA KIJESHI,KUIMARISHA MAFUNZO YA KUJENGA TAIFA NA KUGHARAMIA MAHITAJI MUHIMU KWA ASKARI KAMA MAJI, MAFUTA NA MISHAHARA.

AIDHA AMEBAINISHA CHANGAMOTO AMBAZO MPAKA SASA ZINAIKABILI WIZARA YA ULINZI KUA PAMOJA BAJETI KUTOKUKIDHI MAHITAJI KUTOKA NA MATUMIZI YA WIZARA KUONEKANA KUA MAKUBWA,UPUNGUFU WA ZANA ZA KIJESHI, MAJI UMEME PAMOJA NA MAFUTA.

LICHA YA KUKABILIWA NA CHANGAMOTO HIZO WAZIRI WA ULINZI AMESEMA SERIKALI IMEDHAMIRIA KUREJESHA MAFUNZO YA JKT YATAKAYO HUSISHA WANAFUNZI WATAKAO HITIMU KIDATO CHA SITA AMBAPO MPANGO HUO HAUTAZUI MWANAFUNZI KUENDELEA NA ELIMU YA JUU.

AKIWASILISHA BAJETI HIYO WAZIRI WA ULINZI AMETOA SHUKRANI ZAKE KWA AMIRI JESHI MKUU NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK: JAKAYA MRISHO KIKWETE PAMOJA MAAFISA WENGINE WANGAZI YA JUU WAKIJESHI KWA KUFANIKISHA KUKAMILIKA KWA BAJETI HIYO.

Jul 12, 2011

X-CLUSIVE ENTERTAINMENT NEWS STORY



JULY 12-2012

JUMA NNE SAA TATU USIKU NDANI YA EAST AFRIKAN FLAVER

ZANZIBAR

BAADA YA ILE BIFU YA OFF SIDE TRICK NA MKALI AT KUA GUMZO SANA KOTE NCHINI !!NIKWAMBA MAADUI WA AT WANAZIDI KUJITOKEZA.

KWA SASA KUNA NGOMA MPYA, YA MDUARA TOKA KWA ARTIST JAMILA ABDALLAH ALLY aka BABY J, KUTOKA HAPA NYUMBANI ZANZIBAR, NGOMA AMBAYO PIA AMESHIRKISHWA MSHINDI WA TUZO MBILI ZA ZANZIBAR MUSIC AWARDS 2011 FT GELLY WA RHYMES TOKA USWAZI INAITWA DOMO KAYA

SO NINI KILICHO X-CLUSIVE ZAIDI?? NI KWAMBA KAMA UTAKUMBUKA AT NI MSANII AMBAE ALIFUNGA PINGU ZA MAISHA HIVI KARIBU TU!!NA OFCAUSE DA WIFE OF MY BROTHER NINOMA AISEEE.

LAKINI UKIISIKILIZA KWA MAKINI SAAANA NGOMA HIYO, HUMO NDANI UTASIKIA MISTARI ISEMAYO ''WE UMEOA AU UMEOLEA WENZIO?....INANIKUMBUSHA TRACK YA AT IITWAYO VIFUU TUNDU INASEMA “MWANAMKE MBEYA UTAMJUA TU, MDOMO WAKE MWEUSI KAMA KUNGURU” NA KUMBUKA BABY J ALIPATA SHAVU KWENYE NGOMA YA OFFSIDE TRICK YA KIDUDU MTU.

SO HAPA KUNA AT, OFFSIDE TRICK NA BABY J TENA WOTE TOKA ZANZIBAR KUNANI HAPA NDANI YAKE?!

AU NDIO OFFSIDE TRICK WAMEAMUA TRICK HIYO KUIJIBU VIFU UTUNDU!!!ILI WASIONEKANE MASHOGA MIMI NA WEWE HATUFAHAMU!!

SO!!!! SOTE TUSUBIRI, KAMA KAWAIDA MKALI WA X=CLUSIVE TAKUTAFUTIA HAWA JAMAA NA MWANADADA HUYO, TUWASIKIA WANAMAANISHA NINI KATIKA MISTARI YA MSHAIRI HAYO::

ZANZIBAR

OFACAUSE BIFF MIONGONI MWA WASANII KISIWANI ZANZIBAR ZIKIWA ZINAENDLEA, YES WASANII WENGINE WANAENDELEA KUPIGA HATUA HUKU WAKUPUUZIA BIF HIZO::

HAPA NAMZUNGUMZIA MSANII MIONGONI MWA WASANII WALIOCHUKUA TUZO ZA MWANZO KABISA ZANZIBAR MWAKA 2006 TUZO YA KUNDI BORA

RICO SINGLE.

NINI KILICHO X-CLUSIVE KWAKE NI KWAMBA!!! BAADA YA NGOMA YAKE YA WAFANYAKAZI KUENDELEA KUFANYA VYEMA ZAIDI NA KUZIDI KUMPACHA KATIKA GAME.

RICO SINGLE KESHO ANAONDOKA KISIWANI KUELEKEA JIJINI DAR ES SALAAMA KWA AJILI YA KUFANYA VIDIO YA NGOMA HIYO.

SAMBAMBA NA KUFANYA VIDIO HIYO!!! RICO SINGLE ANAKWENDA KUFANYA NGOMA NYINGINE MPYA AMBAYO ATASHIRIKIANA NA MSANII KUTOKA SALA SALA GODZILA.

INAKUA VIPI KUHU PRODUCTION:: KWA UPANDE WA VIDIO RICO AMESEMA IKO CHINI YA VISIAL LAB LAKINI NGOMA HIYO INAFANYWA KWA USHIRIKIANO WAKE PRODUCER ARO NAME NA KUTOKA JUPITA RECOD PAMOJA NAE MAKOCHARI.

LAKINI KILICHO KIKUBWA ZAIDI KUTOKA KWA MSANII RICO SINGLE!! NIKWAMBA KAMA ULISHA SIKILIZA KWA MAKINI ZAIDI STYLE YA UIMBAJI WAKE NA NAMNA MTU MZIMA ANAVYOJITUPIA KWA MAANA YA PAMBA INASEMEKANA ETI JAMAA HUKOPI SWAGA ZA AY.

OFCAUSE AMEFUNGUKA JUU YA HILO NAKUWEKA WAZI KUA HAKOPI SWAGA ZA MKALI WA KOMESHO ILA NIWASHIKAJI TU WAKARIBU NA WANATUMIA STYLE HIYO YA KOMESHO STYLE KATIKA MUZIKI WAO.

SO ALL DA BEST MY BROTHER TOGATHER TUNAKUTAKIA KAZI NJEMA

.

KUTOKA UGANDA

MOZE NA WEAZEL....WADAIWA HELA YA VIDEO...I!

MOZE RADIO NA WEASEL TV TOKA UGANDA WAMEENDELEZA MISALA COZ JAMAA ANAYEKWENDA KWA JINA LA BASHIR LUKYAMUZI ANAWADAI MKWANJA BAADA YA KUWATENGENEZEA VIDEO YA WIMBO WAO WA LWAKI TOKULA AKA WHY DON'T YOU GROW UP

BASHIR ANADAI KUWA MOZE NA WEAZEL WALILIPA KIASI FLANI CHA FEDHA NA JUMLA YA GHARAMA YA KUFANYA VIDEO HIYO ILIKUA NI SHS MILIONI 3.5 NA WALILIPA NUSU NA WANADAIWA FEDHA ILIYOBAKI.

KINACHOMTIA SHAKA BASHIR NI MUDA WA MIEZI 4 SASA UMEPITA NA BADO HAWAJAMALIZA DENI NA AMETISHIA KUWAPELEKA MAHAKAMANI COZ ANAONA HAKUNA DALILI YOYOTE YA KULIPWA NA KWA SASA AMEGOMA KUFANYA NAO KAZI YOYOTE MPAKA ALIPWE MKWANJA WAKE SHS MILIONI 1.9 ZA UGANDA

Jul 11, 2011

YES ITS ME THE NOMBER ONE IN TOWM






USIULIZE NINI THAT IS MY PROFFESIONAL

NASIPENDI SANA WATU WANAOJIDAI WANAIJUA SANA WAKATI JAMII INAWATAMBUA KUWA HAWAWEZI LOLOTE KUHUSIANA NA TAALUMA HIYO.

OFFCAUSE NIKO MJENGO CHUCHU FM RADIO,

WHAT AM I PERFORM THERE

KARIBU USIKILIZE EAST AFRICAN FLAVER TUKIWASAIDIA VIJANA WA MUZIKI WA BONGO FLAVER KUSHINE HAPA TOWN

LAKINI PIA USIKOSE KUSIKILIZA MAHABARI COZ MTAYARISHAJI NI MIMI MWENYEWE KUSOMA NDIOUSIPIME AISEEEEE.

LAKINI SIKILIZA WAKE UP CALL KUANZIA SAA KUMI NA MBILI ASUBUHI MPAKA SAA NNE ZA ASUBUHI.

NI HAPA HAPA MJENGONI AISEEEEEEEEEEE


HUYO JAMAAA MWENYE MIDEVU NI MKALI SANA KATIKA SPORT AISEEEE JAMAA ANAITWA ISSA ABDURAHMANI NDOKEJI

Jul 10, 2011

YANGA BINGWA MICHUANO YA KAGAME:LAKINI WAANDAAJI WALIANGUSHA TAIFA

KILE KITENDAWILI NANI MKALI HATIMAE KIMETEGUKA BAADA YA MGANYAMA SIMBA HII LEO KUTAFUNWA KAMA ALIVYOZOWEA KUWATAFUNA WENZAKE.

DAKIKA TISINI KATIKA HISTORIA ZILIZIKA PASI KILA MMOJA KUONA LANGO LA MWENZAKE LAKINI MNAMO DADKIKA THELATHINI ZA NYONGEZA YANGA ALIPACHIKA KITU NYAVUNI NA KUFANYA DAKIKA 120 ZA MCHEZO KUMALIZIKA KWA BAO MOJA BILA.

YANGE KWA MARA YA NNE SASA WAMECHUKUA KOMBE HILO LAKINI SAFARII HII WAMELICHUKUA KIZANI BAADA YA UMEME KUSUBIRI WABABE HAO WAKAPEWE MATAJI YAO NDIPO UKATIKE, NAKWELI UKAKATIKA.

YANGA WAMEVALISHWA MATAJI KIZANI,WAPEWA KOMBE KIZANI NA KUFANYA UTAMU WOTE KWA MASHABIKI KUYEYUKA, SITAKI KUSEMA KAMA NI FITINA AU LAH!!

NINI ATHARI ZA UMEME KUKATIKA?KWANZA IMESHUSHA UHAKIKA WAKUAMINIWA KAMA TUTAWEZA KUANDAA MASHINDANO MAKUBWA ZAIDI YA HAYO!

PILI AIBU KWA TAIFA ZIMA KWA SASA BABU NIMATAIFA TAKRIBAI YOTE AFRIKA YALIKUA YANAFUATILIA MCHEZO HUO.

HATUA ZICHUKULIWE KWA UZEMBE ULIOJITOKEZA KATIKA MASHINDANI HAYO VINGIVYO HAMTA WAAMBIA KITU WATANZANIA

SIMBA NA YANGA NANI MBABE LEO

MTANANGE WA SIMBA NA YANGA NDIO LEO, HAKIKA ASILIMIA KUBWA YA MASHABIKI WALIKUA WANAJUA HIVYO KWA HAWA JAMAA LAZIMA WATAKUTANA FAINALI.

KUNA SABABU NYINGI AMBAZO WATU WALIKUWA WAKIZISEMA KUA HAWA JAMAA LAZIMA WAKUTANE KAMA WEWE NI MDAU WA SOKA HAUTO NIULIOZA NI ZIPI.

MOJA NI KWAMBA WAKO HOME

LAKINI PILI WATU WANAITILISHA WANAWATILISHA SHAKA KWA LENGO LA KUTAK A KUJIPAJIPATIA KIPATO KINGI ZAIDI JAPO WAO WATABISHA.

LAKINI TATU KWAMBA HAO NDIO WANAOONGOZA KWA MASHABIKI NCHINI HIVYO LAITI KAMA WANGELITOKA MAPEMA HAKIKA MASHINDANO YASINGELINOGA.

KAZI NI LEO UNADHANI NA ANAOBUKA MSHINDI STAY TUNE

YALIYOJIRI ZANZIBAR

PEMBA

WALIMU, WAZAZI NA WALEZI KISIWANI PEMBA , WAMETAKIWA KUBADILIKA NA KUACHA TABIA YA KUTUMIA BAKORA KATIKA KUWAADHIBU WATOTO NA BADALA YAKE WATUMIE NJIA MBADALA ZILIZOPO AMBAZO ZINAZOWEZA KUMFUNZA NA KUMTIA ADHABU MTOTO ISPOKUWA BAKORA.

WITO HUO UMETOLEWA NA MRATIB WA MARADI WA KUHAMASISHA ADHABU MBADALA MASHULENI, KUTOKA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR , SAFIA ALI RIJALI, WAKATI AKIZUNGUMZA NA MAAFISA ELIMU,WALIMU PAMOJA NA WANAFUNZI KUTOKA SHULE NNE ZA PEMBA.

MRATIB HUYO, AMESEMA KUWA, WALIMU, WAZAZI NA WALEZI WAMEZOEA KUTUMIA BAKORA KATIKA KUWAADHIBU WATOTO JAMBO AMBALO LINALOWEZA KUMFANYA MATOTO KUWA MKAAIDI NA BADALA YAKE SASA WATUMIE ADHABU MBADALA ISPOKUWA BAKORA NA MTOTO ANAWEZA KUFUNDISHIKA.

AIDHA AMESEMA KUWA, BAKORA SIO NJIA NZURI KWA KUREKEBISHA TABIA NA KUWAFANYA WATOTO WAFAHAMU, KWANI ZIPO ADHABU NYINGI ANAZOWEZA KUPATIWA WATOTO, KAMA KUWAPA KAZI NDOGO NDOGO, KUWEKEANA AHADI PALE ATAKAPOFANYA KOSA, KUZUNGUMZA NAO, KWANI BAKORA SIO JAMBO LA KUREKEBISHA TABIA.

MRATIB SAFIA, AMEFAHAMISHA KUWA, LENGO LA MRADI HUO NI KUHAMASISHA WALIMU, WAZAZI NA WALEZI KUACHA KUTUMIA ADHABU YA VIBOKO KWA WATOTO NA BADALA YAKE KUTUMIA ADHABU MBADALA AMBAZO HAZITAWAATHIRI WATOTO KIMWILI, KIAKILI NA KISAIKOLOJIA.

NAYE AFISA MDHAMINI WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI PEMBA, MOH’D IDDI JUMA, AMESEMA KUWA, MATUMIZI YA BAKORA YAMEONEKANA KULETA MADHARA MAKUBWA MASHULENI, IKIWEMO KUSABABISHA ULEMAVU WA VIUNGO KWA BAADHI YA WATOTO.

PIA AMEBAINISHA KUWA, UKOSEFU WA AMANI NA HOFU HUREJESHA NYUMA AMANI NA MAENDELEO YA WANAFUNZI KUTOKANA NA MATUMIZI YA BAKORA, ILI KUWEZA KUONDOSHA HALI HIYO NI KUHAKIKISHA WANANFUNZI WANAPATA ADHABU MBADALA INAYOWAJENGA ZAIDI KITAALUMA NA KUPATA HAKI YAO YA MSINGI ELIMU YA LAZIMA.

 
 
 
 
 
 
 
WILAYA YA KUSINI
 

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 5.5 ZIMEKUSANYWA NA JUMUIA YA MIKOPO NA MAENDELEO YA JOZANI (JOCDO), WILAYA YA KUSINI UNGUJA , IKIWA NI MICHANGO YA WANAVIKUNDI WANACHAMA 437 INAYOJUMUISHA WANACHAMA 11,750.

AKIWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI NA MATUMIZI, KWENYE MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI,AMBAO UMEFANYIKA SKULI YA KITOGANI, NAIBU KATIBU WA JUMUIA HIYO MUSTAFA MAKAME, AMESEMA KUA, KIWANGO HICHO CHA FEDHA KILIKUSANYWA KUANZIA JULAI MWAKA 2007 HADI JUNI 2011.

AMESEMA KUA KATIKA KIPINDI HICHO CHA MIAKA MINE, WANACHAMA WANAWAKE PEKEE WAKIWA NI ELFU TISA MIA MBILI TISINI NA MBILI,WALIKUSANYA KIASI CHA SHILINGI MILION MIA NNE KUNI NA NANE ELFU, LAKI TANO NA ELFU HAMSINI(418, 950, 000),WAKATI KWA UPANDE WA WANAUME WAKIWA NI ELFU MBILI MIANNE HAMSINI NA NANE (2,458), WAMEKUSANYA JUMYA YA HISA MILION HAMSINI NA TATU, LAKI NANE NA TISINI NA MOJA ELFU.(53,891, 000).

KUFUATIA MAKUSANYO HAYO, JUMUIA IMEWEZA KUTOA MIKOPO YENYE THAMANI YA SHILINGI MILION MIANANE ISHIRINI NA SITA,LAKI NANE NA THELATHINI NA NNE ELFU (826,834,000) ,NA WANAWAKE WALIOBAHATIKA WALIKUA NI ELFU SITA MIATISA THELATHINI (6,930), WAKATI WANAUME WALIKUWA ELFU MOJA MIA TATU SABINI NA MOJA(1,371), KUTOKA VIKUNDI MBALI MBALI VYA WILAYA TANO ZA UNGUJA.

MPEMA AKIFUNGUA MKUTANO HUO ULIOAMBATANA NA UCHAGUZI ,MKUU WA WILAYA YA KUSINI HAJI MKUNGU MGONGO, AMEWATAKA VIONGOZI WA VIKUNDI MBALI MBALI, MBAVYO NI WANACHAMA WA JUMUIA HIYO YA JOCDO, KUWAHARAKISHA WANANCHAMA WAO ILI KUREJESHA MIKOPO.

KATIKA UCHAGUZI HUO VIZAA MAKONDE MONDI AMECHAGULIWA KUA KATIBU MKUU, JUMA SULEIMAN KHAMIS MWENYEKITI, NA MAKAMU WAKE SAID DUDE KHATIB PAMOJA NA WAJUMBE SITA WA KAMATI MAALUM YA WANANWAKE.