Jul 14, 2011

DODOMA

WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROF. PETER M. MSOLLA, HII LEO AMEWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2010/2011 YENYE ZAIDI YA SHILINGI BILIONI SITINI NA NNE MILIONI MIAMOJA KUMI NA SABA NA LAKI TANO SITININA MBILI ELFU.

KWA MUJIBU WA WAZIRI MSOLLA, MAMBO AMBAYO AMESEMA YATAPEWA KIPAUMBELE KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI HIYO, NI PAMOJA NA KUMALIZIA UKARABATI WA MAJENGO YA VYUO VYA SAYANSI NA TEKNOLOJIA HAPA NCHINI ILI KUSAIDIA KUONGEZA IDADI YA WATAALAM KATIKA SEKTA HIYO.

PIA SERIKALI IMEPANGA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA SUALA LA UTAFIKTI KUTOKANA NA NCHI KUWA NYUMA KATIKA SUALA HILO, AMBAPO HATUA AMESEMA MPAKA SASA HATUA KADHAA ZIMEKWISHA ANZA KUTEKELEZWA.

AIDHA AMEIAMBIA SERIKALI KUA WIZARA YAKE INAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA YA UKOSEFU WA RASILIMALI WATU, AMBAPO WIZARA YAKE KWA KUSHIRIKIANA NA TUME AMESEMA IMEJIWEKEA MKAKATI WA KUHAKIKISHA WANAHAMASIHA WATU KUSOMA MASOMO YA SAYANSI ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIYO.

LICHA YA CHANGAMOTO HIZO WAZIRI MSOLLA AMESEMA SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO ILI KUBORESHA HUDUMA ZA MAWASILIANO, AMBAPO AMETHIBITISHA KUA ZANZIBAR ITAUNGANISHWA KWENYE MKONGO HUO MARA BAADA YA KUKAMILIKA.

WILAYA YA MJINI UNGUJA

KITUO CHA KUWAENDELEZA VIJANA KIELIMU NA KITAALUMA(STON TOWN YOUTH CENTER), KIMEKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIREJA NYUMA MAENDELEO YA KIYUO HICHO.

HAYO YAMEELEZWA NA MRATIBU WA MRADI WA VIJANA ,JACKSON OGOTU WAKATI AKIZUNGUMZA NA CHUCHU FM OFISINI KWAKE KIKWAJUNI WILAYA YA MJINI ZANZIBAR.

JACKSON AMESEMA KITUO HICHO HUTOWA ELIMU TOFAUTI KWA VIJANA WA RIKA ZOTE, INGAWA KITUO HICHO KUWA NA WAFADHILI LAKINI KINAKABILIWA NA MATATIZO MBALIMBALI ,IKIWEMO UHABA WA FEDHA KWA AJILI YA KUENDELEZA MIPANGO WALIYOYAKUSUDIA.

AIDHA JACKSON AMEFAHAMISHA KUWA KITUO HICHO KIMEJIWEKEA MALENGO TOFAUTI KAMA KUWAKWAMUA VIJANA KIELIMU NA KITAALUMA NA, ILI KUWEZA KUFAIDIKA NA KUONDOKANA NA HALI NGUMU YA KIMAISHA.

SAMBAMBA NA HAYO AMEWATAKA VIJANA KWENDA KUJIUNGA NA KITUO HICHO NA KUACHA TABIA YA KUKAA MASKANI NA KUFANYA MAMBO YASIYOFAA KWA JAMII.


No comments:

Post a Comment