Jul 27, 2011

ZANZIBAR

UAMUZI WA SHIRIKA LA KUDHIBITI NISHATI NA MAJI (EWURA), KUCHUKUA JUKUMU LA KUIUZIA ZANZIBAR UMEME BADALA YA SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO), UMEWACHAFUA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI NA KUIOMBA SERIKALI KULISHITAKI SHIRIKA HILO .

WAWAKILISHI HAO WAMETOA KAULI HIYO BAADA YA KUPOKEA BAJETI YA WIZARA YA BIASHARA VIWANDA NA MASOKO, ILIYOWASILISHWA HII LEO NA WAZIRI NASSOR AHMED MAZRUI KWA WAJUMBE WA BARAZA HILO KISIWANI ZANZIBAR.

AKIWASILISHA BAJETI HIYO WAZIRI MAZRUI, AMESEMA KATIKA UKAGUZI WALIOUFANYA KWA BAADHI YA VIWANDA WAMEBAINI VINAKABILIWA NA MATATIZO MENGI IKIWEMO UKUBWA WA GHARAMA ZA UMEME.

MWAKILISHI WA WETE ASAA OTHMAN HAMAD, AMESEMA SERIKALI INAPASWA KUTOLIVUMILIA SHIRIKA HILO NA IPO HAJA KWA WAZIRI WA NISHATI ZANZIBAR KUIFUNGULIA MASHTAKA TAASISI HIYO.

AIDHA AMESEMA ZANZIBAR ILIPOTAKA KUTUMIA HUDUMA ZA SHIRIKA HILO ILIFANYA MAKUBALIANO NA TANESCO NA SIO EWURA.

HUO UMETAJWA KUWA UKIUKWAJI MKUBWA WA MKATABA WA UNUNUZI WA HUDUMA HIYO, NA HAKUNA HAJA YA KUNUNULIWA KATIKA DUKA LA REJAREJA WAKATI MAKUBALIANO NI KUFANYA MANUNUZI KATIKA DUKA LA JUMLA.

AMELISHUTUMU SHIRIKA HILO KUWA PENGINE LINAFANYA HIVYO MAKUSUDI ILI KUWAKATISHA TAMAA WATUMIAJI WA HUDUMA HIYO, HATUA INAYOFANYA WATU WENGI WASHINDWE KUUNGANISHA UMEME MAJUMBANI KWA UKUBWA WA GHARAMA SAMBAMBA NA BAADHI MIRADI KUKWAMA.

MWAKILISHI HUYO AMESHAURI WIZARA HIYO IIFUNGULIE MASHTAKA EWURA KWANI SHIRIKA HILO SILO LENYE MAMLAKA YA KUIUZIA UMEME ZANZIBAR NA KUFANYA BIASHARA HIYO NI KINYUME CHAA SHERIA.

WILAYA YA MJINI


WAKATI MATAIFA YA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA PEMBEZONI MWA AFRIKA YAKIKABILIWA NA NJAA, KISIWA CHA ZANZIBAR KIMETAJWA KUWA SALAMA NA HALI HIYO.

KWA MUJIBU WA TAASISI YA THE
FAMINE EARLY WARNING SYSTEMS NETWORK (FEWSNET) YA MAREKANI KATIKA RIPOTI YAKE IMEITAJA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMBAYO INAJUMUISHA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA KUWA HAIMO KATIKA TISHIO LA NJAA.

TAASISI HIYO AMBAYO IMEKUWA IKIANGALIA HALI YA CHAKULA DUNIANI IMETOA TAARIFA INAYOONYESHA KUWA BARA LA AFRIKA NDILO LIMEATHIRIWA ZAIDI NA UKAME AMBAPO NCHI NYINGI ZA PEMBE YA AFRIKA ZITAKABILIWA NA HALI MBAYA YA CHAKULA.

KATIKA RIPOTI HIYO IMEZITAJA NCHI ZA KENYA, ETHIOPIA NA SOMALIA KUWA KUNA BAADHI YA MAENEO YA NCHI HIZO YAMEATHIRIWA VIBAYA NA UKAME NA KWAMBA YANAHITAJI MSAADA WA HARAKA WA CHAKULA KUNUSURU MAISHA YA WANANCHI WAKE AMBAO WAMEKUWA HAWAPATI CHAKULA KWA WAKATI.

KATIKA MKUTANO WAKE WA DHARURA ULIOFANYIKA JIJINI ROME, ITALIA, SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA MPANGO WA CHAKULA(WFP) LIMEZITAJA NCHI AMBAZO ZINAKABILIWA NA HALI MBAYA YA CHAKULA KWA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA PEMBE YA KASKAZINI YA AFRIKA KUTOKANA NA UKAME NI BURUNDI, JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO, MADAGASCAR, MSUMBIJI, SUDAN, ETHIOPIA, SOMALIA NA UGANDA.

WAZIRI WA KILIMO NA MALIASILI WA ZANZIBAR, MANSOOR YUSSUF HIMID AMESEMA UMAKINI WA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, DK ALI MOHAMMED SHEIN KATIKA KUSIMAMIA UHAKIKA WA CHAKULA NA KUSHAJIISHA KILIMO CHENYE TIJA UMESAIDIA SANA KUIONDOA ZANZIBAR KATIKA ORODHA YA NCHI ZENYE NJAA.


WIILAYA YA MAGHARIBI

WITO UMETOLEWA KWA MADEREVA NA MAKONDA WA GARI ZA ABIRIA KISIWANI ZANZIBAR, KUFUATA TARATIBU ZA UVAAJI WA SARE UNAOTARAJIWA KUANZA TAREHE MOJA MWEZI WA NANE MWAKA HUU.

WITO HUO UMETOLEWA NA MKURUGENZI WA IDARA YA USAFIRI NA LESENI SULEIMAN KIROBO WAKATI AKIZUNGUMZA NA CHUCHU FM OFISINI KWAKE MWANAKWEREKWE WILAYA YA MAGHARIB UNGUJA.

AIDHA SULEIMAN AMESEMA MADEREVA NA MAKONDA WOTE WA UNGUJA NA PEMBA WANATAKIWA KUVAA SARE AINA YA SUTI ZILIZO ANDALIWA KWA KILA WILAYA.

SULEIMAN AMESEMA UTARATIBU HUO NI VYEMA UKAZINGATIWA NA WAHUSIKA KWANI ATAKAE BAINIKA KUKIUKA UTARATIBU HUO ATATOZWA FAINI YA ZAIDI YA SHILINDI ELFU 10, NA AKISHINDWA KULIPA FAINI HIYO ATAFUATA MASHARTI ATAKAYOPEWA NA MAHAKAMA.

SAMBAMBA NA HAYO SULEIMAN AMEWATAKA ASKARI WA USALAMA BARABARANI KUWA WAADILIFU KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI HILO LINATEKELEZWA KIKAMILIFU ILI KUFIKIA MALENGO WALIYOYAKUSUDIA.

DAR ES SALAAM

TAASISI YA WANAWAKE NA MAENDELEO (WAMA) KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA AFYA LAKIMATAIFA (FHI) PAMOJA TUWALE, ZIMEUNDA KAMATI MBILI ZITAKAZO FANYA KAZI YA KUWAKOMBOA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI KWA KUTEKELEZA KAMPENI ZA USHAURI NA UTETEZI KWA WATOTO HAO.

HAYO YAMEELEZWA NA AFISA TATHIMINI NA UFUATILIAJI WA WAMA GLORIA MINJA WAKATI AKIONGEA NA WAJUMBE WA KAMATI HIZO AMBAZO NI KAMATI YA WATOTO WANAOTOKA KATIKA MAZINGIRA HATARISHI NA KAMATI YA WADAU MBALIMBALI KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA GRAND VILLA JIJINI DAR ES SALAAM .

JUMLA YA WAJUMBE SITA WANATARAJIWA KUTOKA KATIKA KAMATI YA WATOTO WANAOTOKA KATIKA MAZINGIRA HATARISHI NA KAMATI YA WADAU MBALIMBALI ITAKUWA NA WAJUMBE NANE KUTOKA SERIKALI KUU AMBAYO NI WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO NA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII , HALMASHAURI ZA WILAYA, MANISPAA NA MIJI, ASASI ZA KIRAIA, VYOMBO VYA HABARI, SEKTA BINAFSI NA WAFANYAKAZI WA WAMA NA FHI.

LENGO KUBWA LA MRADI HUO NI KUBORESHA HALI YA MAISHA YA WATOTO HAO, HASA WATOTO WA KIKE NA KAYA ZAO KWA KUWAJENGEA UWEZO WANAKAYA NA JAMII ILI WATOE HUDUMA KAMILIFU, BORA NA ENDELEVU KWA WATOTO HAO NA UTAKUWA TOFAUTI NA MIRADI MINGINE AMBAYO INASHUGHULIKA NA MTOTO.

AIDHA, MINJA AMESEMA KUWA WAJUMBE WA MRADI HUO WATAWEZA KUFAHAMU MRADI WA PAMOJA TUWALEE JINSI UNAVYOFANYA KAZI NA MIPANGO YA KAMPENI ZA USHAWISHI NA UTETEZI KWA WATOTO WANAISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI.

DODOMA

WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI DK. DAVID MATHAYO DAVID, HII LEO AMEWASILISHA BUNGENI BAJETI YA MAKADIRIO YA MATUMIZI NA MAPATO YA WIZARA YA HIYO YENYE JUMLA YA SHILINGI BILIONI 57.1 KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012.

BAADHI YA MAMBO MUHIMU YALIYOPATIWA KIPAUMBELE KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI HIYO, NI UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UVUVI WENYE LENGO LA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI WA VIUMBE VYA MAJINI NA MAZINGIRA KWA WAVUVI.

KUTEKELEZA AHADI ILIYOTOLEWA NA SERIKALI KWA WAFUGAJI WALIOATHIRIWA NA UKAME KWA BAADHI YA MIKOA YA KILIMANJARO, ARUSHA NA MANYARA AMBAPO JUMLA YA SHILINGI BILIONI 8.7 ZIMETENGWA NA SERIKALI KWA AJILI YA MALIPO HAYO.

WAZIRI DAVIDI MATHAYO AMETOA WITO KWA SEKTA BINAFSI KUJITOKEZA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA UVUVI, AMBAPO SERIKALI IMEENDELEA KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA HIYO, KWA KUONDOA KODI KWENYE NYUZI ZA KUTENGENEZEA NYAVU ZA UVUVI NA KUONDOA MRAHABA KWA UVUVI WA MAJINI.

AKIZUNGUMZIA SUALA LA ULAJI WA NYAMA NA UNYWJI WA MAZIWA WAZIRI AMESEMA KWA SASA SERIKALI INAENDELEA NA MATAYARISHO YA UJENZI WA MACHINJIO YA KISASA ITAKAYO KAMILIKA MWAKA HUU WA FEDHA 2011/2012 NA ITAENDELEA KUHIMIZA UWEKEZAJI ILI KUHAKIKISHA UZALISHA WA MAZIWA UNAONGEZEKA.

AIDHA WAZIRI AMETOA SHUKRA ZAKE KWA WAHISANI NA WADAU WOTE AMBAO WAMEKUA WAKICHANGIA KATIKA MAENDELEO YA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI IKEWEMO MAREKANI, JUMUIA ZA AFRIKA MASHARIKI NA JAPAN.

Jul 25, 2011

MTWARA

TANZANIA IKIWA INAELEKEA KUADHIMISHA MIAKA HAMSINI YA UHURU MWEZI SEPTEMBER MWAKA HUU, HII LEO IMEADHIMISHA SHEREHE YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA 109, WALIOFARIKI WAKIPIGANIA UHURU HUO, AMBAPO KITAIFA SHEREHE HIZO ZIMEFANYIKA NALIENDELE MKOANI MTWARA,MGENI RASMI AKIWA NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK.JAKAYA MRISHO KIKWETE.

MIONGONI MWA SHUGHULI MUHIMU ZILIFANYIKA KATIKA MAADHIMISHO HAYO, NI UWEKAJI SILAHA ZA ASILI PAMOJA NA KUVALISHA MASHADA YA MAUA KATIKA MNARA WA KUMUKUMBU, NA JUMLA YA MIZINGA 21 ILIPIGWA KUTOA HESHIMA KWA MASHUJA HAO.

AIDHA RAIS KIKWETE, ALITEMBELEA MABANDA YA MAKUMBUSHO AMBAYO HUTUMIKA KUTUNZA KUMBUKUMBU YA ZANA ZA KIVITA, ZILIZOTUMIWA WAKATI WAKUPIGANIA UHURU NA MARA BAADA YA KUMALIZA VIONGOZI WADINI ZOTE WALIOMBA DUA KUWAOMBEA MASHUJAA HAO.

AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI NA WANANCHI WALIOHUDHURI KATIKA MAADHIMISHO HAYO, RAIS KIKWETE AMESEMA WATANZANIA WANAPASWA KUIENZI NA KUEHESHIM SIKU YA MASHUJAA, KUTOKANA NA MCHANGO MKUBWA ULIOTOLEWA NA MASHUJAA HAO KATIKA HARAKATI ZA UKOMBOZI WA TAIFA HILI NA MATAIFA MENGINE BARANI AFRIKA.

MAADHIMISHO HAYO PIA YAMEHUDHURUIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKITAIFA, AKIWEMO MAKAMU WA RAIS DK.MOHAMED GHALIB BILALI NA RAIS WANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN NA MKUU WA MAJESHI YA TANZANIA DIVIS MWAINYANGE.

KWA UPANDE WAKE DK.SHEIN AKIILISHA ZANZIBAR AMETOA SHUKRANI ZAKE ZA DHATI KWA NIABA YA WANANCHI WA KATIKA KUADHIMISHA SHEREHE HIYO.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA HUFANYIKA KILA MWAKA JULY 25 KUWAENZI MASHUJAA WALIOPIGANIA UHURU WA NCHI YETU NA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU ULIOPO.