Jul 13, 2011

FAHAMU HILO KUTOKA BUNGENI NA ZANZIBAR

WILAYA YA KUSINI UNGUJA

MKUU WA WILAYA YA KUSINI UNGUJA HAJI MAKUNGU MGONGO AMEWAAHIDI WAKULIMA WA KIJIJI CHA MTENDE NA KIZIMKAZI DIMBANI KUA, ATASHIRIKIANA NA WIZARA YA KILIMO NA MALI ASILI, ILI KUHAKIKISHA WAKULIMA WANAPATA DAWA ZA KUUWA WADUDU WAHARIBIFU.

AMEYASEMA WAKATI AKIWA KATIKA ZIARA YAKE UZINDUZI WA KILIMO CHA MOGOMBA NA UVUNAJI WA MPUNGA KATIKA KIJIJI CHA KIZIMKAZI NA MTENDE WILAYA YA KUSINI UNGUJA.

AIDHA HAJI AMEWAPONGEZA WAKULIMA HAO KWA JITIHADA ZAO WALIZOZIFANYA KATIKA KUFANIKISHA KILIMO CHA MPUNGA NA KUAHIDI KUWA, ATAFANYA JITIHADA ZA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA KILIMO KUHAKIKISHA WANAPATIWA DAWA ZA WADUDU WAHARIBIFU ILI KUNUFAIKA NA KILIMO.

KWA UPANDE WAO WAKULIMA, WAMESEMA PAMOJA NA JITIHADA ZOA ZOTE ILA BADO WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO NYINGI AMBAZO ZINAHIJI KUPATIWA UFUMBUZI, ILI NAOWAWEZE KUFIKIA MALENGO WALIYOYAKUSUDIA.

PAMOJA NA HAYO WAMEIOMBA WIZARA YA KILIMO KUWA KARIBU NAO, ILI KUWEZA KUJUA MATATIZO YANAYO WAKABILI KATIKA KUENDELEZA KILIMO KWA LENGO LA KUNUFAIKA NA UKULIMA WAO.

DODOMA

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LAKUJENGA TAIFA DAKTARI HUSEEN ALLY MWINYI, HII LEO AMEWASILISHA BUNGENI BAJETI YA MAKADIRIO YA MATUMIZI NA MAPATO YA WIZARA YAKE, INAYOTARAJIWA KUTUMIA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MIASITA THEMANINI NA MBILI, BILIONI MIATATU THEMANINI NA TANO NA MIAMOJA ARUBAINI NA TANO ELFU KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012.

AKIBAINISHA MAMBO YALIYOPEWA KIPAUMBELE KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI HIYO, DK: HUSSEN AMESEMA WIZARA YAKE IMEPANGA KUAJIRI WANAJESHI WAPYA NA KUIMARISHA MAFUNZO YA KIJESHI,KUIMARISHA MAFUNZO YA KUJENGA TAIFA NA KUGHARAMIA MAHITAJI MUHIMU KWA ASKARI KAMA MAJI, MAFUTA NA MISHAHARA.

AIDHA AMEBAINISHA CHANGAMOTO AMBAZO MPAKA SASA ZINAIKABILI WIZARA YA ULINZI KUA PAMOJA BAJETI KUTOKUKIDHI MAHITAJI KUTOKA NA MATUMIZI YA WIZARA KUONEKANA KUA MAKUBWA,UPUNGUFU WA ZANA ZA KIJESHI, MAJI UMEME PAMOJA NA MAFUTA.

LICHA YA KUKABILIWA NA CHANGAMOTO HIZO WAZIRI WA ULINZI AMESEMA SERIKALI IMEDHAMIRIA KUREJESHA MAFUNZO YA JKT YATAKAYO HUSISHA WANAFUNZI WATAKAO HITIMU KIDATO CHA SITA AMBAPO MPANGO HUO HAUTAZUI MWANAFUNZI KUENDELEA NA ELIMU YA JUU.

AKIWASILISHA BAJETI HIYO WAZIRI WA ULINZI AMETOA SHUKRANI ZAKE KWA AMIRI JESHI MKUU NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK: JAKAYA MRISHO KIKWETE PAMOJA MAAFISA WENGINE WANGAZI YA JUU WAKIJESHI KWA KUFANIKISHA KUKAMILIKA KWA BAJETI HIYO.

No comments:

Post a Comment