Jul 15, 2011

KUTOKA MJENGONI DODOMA ILIKUA HIVI

DODOMA

KAMATI YA NISHATI NA MADINI, HII LEO IMEITAKA SERIKALI YA JAMHURUI YA MUUNGANO WA TANZANA, KUTOA MAELEZO YATAKAYO JITOSHELEZA KUHUSIANA NA MAAMUZI YAKE YA UNUNUZI WA MTAMBO MKUBWA WA KUZALISHA UMEME ULIO NA GHARAMA, HALIYAKUA SERIKALI HAINA GESI YA KUTOSHA YA KUUENDESHEA MTAMBO HUO.

KAULI HIYO IMETOLEWA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI JANUARI MAKAMBA, WAKATI AKIWASILISHA TAARIFA YA MAKADIRIA NA MAPATO YA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI YA MWAKA 2011/2012.

HATUA HIYO IMEKUJA BAADA YA KAMATI YA NISHATI NA MADINI KUBAINI KUONGEZEKA KWA GHARAMA ZA UZALISHAJI WA UMEME KWA SERIKALI, HUKU TATIZO LA UPATIKANAJI WA UMEME KWA WANANCHI WAKE LIKIZIDI KUONGEZEKA.

AIDHA KAMATI HIYO IMEITAKA SERIKALI KUTAMBUA KUA, UPUNGU WA MVUA HAUWEZI KUA SABABU KUBWA YA TATIZO LA UPATIKANAJI WA UMEME, HALI YAKUA NCHI INAJITOSHELEZA KWA KUA NA VYANZO VINGI VYA KUZALISHA NISHATI YA UMEME.

PAMOJA NA HAYO, KAMATI HIYO IMEISHAURI SERIKALI KUONGEZA JUHUDI ZAKE KATIKA KUWEKEZA KWENYE VYANZO HIVYO MBADALA VYA KUZALISHA UMEME PAMOJA NA KUUJUMUISHA MPANGO WA DHARULA WA TAIFA WA UPATIKANAJI WA UMEME KATIKA MPANGO WA MIAKA MIRTANO ULIOPITISHWA NA SERIKALI.

JANUARI MAKAMBA AMEWASILISHA MAKADIRIA NA MAPATO YA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI YA MWAKA 2011/2012, YENYE ZAIDI YA SHILINGI BILONI 402 NA MILIONI 412, AMBAZO ZIMEPINGWA NA MWAKILISHI WA KAMBI YA UPINZANI JOHN MNYIKA, WAKIITAKA SERIKALI IPUNGUZE BAJETI HIYO KUTOKANA NA MATUMIZI MABAYA YA ANASA YANAYOFANYWA NA BAADHI YA WATUMISHI WA WIZARA HIYO, HUKU WAKIWAACHA WACHIMBAJI WADOGOWADOGO MIGODINI WAKIFA NJAA

No comments:

Post a Comment