Jul 13, 2011

ROSTAM AZIZI MBUNGE WA IGUNGA AJIVUA GAMBA


Taarifa zilizotufikia kutoka Igunga Tabora kupitia kutuo cha Televisheni cha ITV zinasema Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa NEC wa chama cha mapinduzi CCM Rostam Azizi, amejiouzulu nyazifa zake hizo ambazo alikuwa nazo katika Chama cha mapinduzi CCM ambapo kwa sasa anaongea na wananchi wa jimbo hilo .

Mtangazaji wa ITV Samweli Kabendera ameripoti moja kwa moja kutoka Tabora akielezea juu ya tukio hilo, ambalo limetokea muda mfupi uliopita, gazeti moja liliripoti leo kuwa kipindi cha miezi mitatu kilichotangazwa na CCM kwa wanachama wake na viongozi kujivua gamba tayari kimefikia ukomo Hivyo tukio hili inawezekana ndiyo mwendelezo wa CCM kuchukua hatua za kujivua gamba ili kurejesha imani kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.

No comments:

Post a Comment