Dec 17, 2013
MKAZI WA MOSHI AKABIDHIWA JENERETA YAKE YA WEKA UPEWE YA NBC
Rais Kikwete afungua mkutano wa TNBC jijini Dar es Salaam leo
Chini akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo*
*Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya Tanzania National Business Council muda mfupi kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa TNBC uliofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo
Nov 15, 2013
Aug 21, 2013
HII ILIKUWA NI SIKU YA MAFUNZO KWA WANAHABARI MKOANI RUVUMA
Shukrana Masinga wa redio Jogoo fm akielekezana jambo na mwenzake
Enes mwaisakila akifuatilia mafunzo kwa umakini wa hali ya juu
HABARI TOKA RUVUMA SONGEA
Baadhi ya
wananchi wa manispaa ya Songea wamewataka viongozi ambao wanachaguliwa na
wananchi kufanyakazi kwa uhadilifu na sio kwenda kinyume na ahadi ambazo
wanazitoa wakati wa kampeni zao.
wameeleza
kuwa lengo la wananchi kuwachagua viongiozi ni kuhitaji kuwawakilishia kero zao
serikalini na kuweza kupatiwa ufumbuzi wake.
Kwa
upande wa viongozi wa vyama vya siasa Mkoa wa Ruvuma wao wamewaomba viongozi
ambao wanaenda kinyume na kazi walizotumwa na wananchi kujiudhuru ili kuwapisha
viongozi ambao watawatekelezea wananchi mahitaji yao.
hivi jana
Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri
na kupangua idara zilizokuwa zikisimamiwa na wizara mbalimbali na kuunda wizara
mpya nne visiwani humo.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Wanachi
wa kijiji cha njala matata kilichopo kata ya mkongo wilaya ya namtumbo wamesema
tatizo la ukosefu wa maji safi na salama katika kijiji hicho linawathiri kwa
kiasi kikubwa wanawake ambao wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta maji .
wamesema
kijiji hicho kina vyanzo vingi vya maji lakini vimekuwa vikipekwa maeneo
mengine tofauti na maeneo wanayoishi na kuitska serikali kuangali jambo hilo
kwa kina kutokana na adha kubwa wanayoipata ya ukosefu maji safi na salama.
wasemema
kuwa kutokana na ukosefu huo wa maji kijijni hapo unaweza kusababisha magonjwa
ya milipuko na matumbo ya kuhara.
Aug 19, 2013
WAKALI WA SAYARI YETU NA AFRIKA YETU 93.0
Mfaume Pastory na Catherine Shayo ni watangazaji wa kipindi cha AFRIKA YETU ndani ya 93.0 ya Jogoo FM Songea kwani sisi ni wa AFRIKA halisi karibu sana kuisikiliza show yetu kila siku za Juma Pili saa nane kamili mmchana hadi saa kumi kamili jioni.
Lakini ni watangazaji wa kipindi mahiri cha SAYARI YETU cha Jogoo FM ambacho hurushwa kila siku za wiki juma tatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa kumi na mbili kamili jioni........JISIKIE FAHARI, KUISIKILIZA SAYARI .
WAKALI WA KIPINDI CHA SAYARI NA AFRIKA NA AFRIKA YETU YA 93.0 MOTO CHINI
TIMU nzima ya kipindi cha AFRIKA YETU ya 93.0 Jogoo Fm kulia Papaa Ramso mutu yenyekujua lighu mingi1!! Ni mtafsri wa nyimbo za kongo anajua lingala, France nk....anafuata ni Catherine shaya Mama wa Afrika yetu na Papaa Mufaume, Paster....Muzee matata wa Afrika yetu......Lakini ni watangazaji wa kipindi mahiri cha SAYARI YETU cha Jogoo FM ambacho hurushwa kila siku za wiki juma tatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa kumi na mbili kamili jioni........JISIKIE FAHARI, KUISIKILIZA SAYARI .
Tuko na mtu wetu anae tuhakikishia usalama wetu bwana
HABARI TOKA RUVUMA TANZANIA
Diwani wa kata ya misufini Salum Mfamaji ambaye pia ni mjumbe wa baraza la
katiba manispaa ya songea amewataka wajumbe ambao wanajadili rasimu ya katiba
kwa manispaa ya songea kujadili mawazo
ambayo yametolewa na wananchi na sio kwa manufaa ya vyama vyao.
Amesema ni lazima wajumbe ambao wamechaguliwa na wananchi kuwawakilisha
wananchi wao kikamilifu badala ya kuangalia maslahi yao binafsi.
Wajumbe wa mabaraza ya mabadiliko ya katiba manispaa ya songea leo wameanza
kujadili rasimu iliyopendekezwa na wananchi kwenye mchakato wa kupata maoni ya
katiba mjadala ambao utakuwa wa siku tatu kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu
matogoro.
Wizara ya
Afya na Ustawi wa jamii imeombwa kuanzisha kliniki katika hospitali na vituo
vya Afya nchini kwa ajiLi ya walemavu wa ngozi Albino walio athirika na ugonjwa
wa saratani ya ngozi ili waathirika hao waweze kutambulika na kupatiwa tiba
badala ya kuwapatia dawa za kuzuia mionzi ya jua.
Mwenyekiti
wa chama cha Albino nchini Ernest Kimaya ameitaka idara ya ustawi wa jamii
kuandaa bajeti itakayosaidia Maalbino nchini kupata huduma ya afya stahiki.
Aidha
kimaya amesema kuwa hadi hivi sasa tayari wamesha fanya mazungumzo na wizara na
wameanza kutoa dawa ya kuzuia mionzi ya jua katika sehemu mbali mbali nchini.
Wachimbaji
wadogo wa madini katika mgodi wa Mererani jijini Arusha wameitaka serikali kusikiliza madai yao kama
wanavyowasikiliza wawekezaji kutoka nje.
Mmoja wa
wachimbaji hao wadogo Jackson Manjuu amesema pindi wanapokuwa na mgogoro baina
yao na wawekezaji huonekana kuegemewa au kupendelewa zaidi kwa wawekezaji bila
kuwajali wachimbaji wadogo ambao ni wazawa.
Manjuu
amesema kuwa ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima serikali haina budi kutenga
maeneo maalumu kwa ajili ya wazawa.
Aug 3, 2013
HABARI KUTOKA RUVUMA
KUTOKA SONGEA RUVUMA TANZANIA
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki amewata wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pindi wanapowaona watu wahalifu ambao wanaenda kinyume na sheria katika jamii inayowazunguka.
Amesema jeshi la polisi limejipanga kudhibiti vitendo vya uhalifu ambavyo vinaendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali yaliyopo ndani ya mkoa.
INSERT..............KAMANDA SAUTI.
Ameyasema hayo baada ya jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa wa makambi uliopo manispaa ya songea kumshikilia mwaharifu ambaye amekutwa na risasi kumi za silaa aina ya SMG anayejulikana kwa jina Mhamed mhamed mwenye umri wa miaka arobaini.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Katibu wa umoja wa wanawake wilaya ya Songea vijijini UWT Selina Ngonyani amewataka wanaume kutoa ushirikiano kwa familia zao kwa kutoa huduma zote za msingi ambazo zinahitajika katika familia zao.
amesema wazazi wote washirikiane kwa pamoja kwa kupangilia kipato ambacho wanakipata katika msimu huu wa mavuno ili waweze kuberesha maendeleo ya pamoja katika familia zao wanazoishi.
INSERT........UWT SAUTI.
Kwa upande wa mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM songea vijijini Nely Duwe amesema wazazi wote hawana budi kushirikiana ili kuweza kupata maendeleo kwa kusomesha watoto wao na kuberesha maisha yao.
INSERT..............MWENYEKITI SAUTI.
Kwa upande mwingine wamewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo wamepewa wananchi waliojiunga katika vikundi mbalimbali katika jimbo la peramiho waliyopewa na Mbunge wa jimbo la Peramiho Jenestha Mhagama ukiwemo mradi wa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.

Apr 28, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)