Aug 21, 2013

HABARI TOKA RUVUMA SONGEA




Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Songea wamewataka viongozi ambao wanachaguliwa na wananchi kufanyakazi kwa uhadilifu na sio kwenda kinyume na ahadi ambazo wanazitoa wakati wa kampeni zao.

wameeleza kuwa lengo la wananchi kuwachagua viongiozi ni kuhitaji kuwawakilishia kero zao serikalini na kuweza kupatiwa ufumbuzi wake.

Kwa upande wa viongozi wa vyama vya siasa Mkoa wa Ruvuma wao wamewaomba viongozi ambao wanaenda kinyume na kazi walizotumwa na wananchi kujiudhuru ili kuwapisha viongozi ambao watawatekelezea wananchi mahitaji yao.

hivi jana Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kupangua idara zilizokuwa zikisimamiwa na wizara mbalimbali na kuunda wizara mpya nne visiwani humo.

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Wanachi wa kijiji cha njala matata kilichopo kata ya mkongo wilaya ya namtumbo wamesema tatizo la ukosefu wa maji safi na salama katika kijiji hicho linawathiri kwa kiasi kikubwa wanawake ambao wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta maji .

wamesema kijiji hicho kina vyanzo vingi vya maji lakini vimekuwa vikipekwa maeneo mengine tofauti na maeneo wanayoishi na kuitska serikali kuangali jambo hilo kwa kina kutokana na adha kubwa wanayoipata ya ukosefu maji safi na salama.

wasemema kuwa kutokana na ukosefu huo wa maji kijijni hapo unaweza kusababisha magonjwa ya milipuko na matumbo ya kuhara.



No comments:

Post a Comment