Aug 21, 2013

HII ILIKUWA NI SIKU YA MAFUNZO KWA WANAHABARI MKOANI RUVUMA


Shukrana Masinga wa redio Jogoo fm akielekezana jambo na mwenzake





Enes mwaisakila akifuatilia mafunzo kwa umakini wa hali ya juu

HABARI TOKA RUVUMA SONGEA




Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Songea wamewataka viongozi ambao wanachaguliwa na wananchi kufanyakazi kwa uhadilifu na sio kwenda kinyume na ahadi ambazo wanazitoa wakati wa kampeni zao.

wameeleza kuwa lengo la wananchi kuwachagua viongiozi ni kuhitaji kuwawakilishia kero zao serikalini na kuweza kupatiwa ufumbuzi wake.

Kwa upande wa viongozi wa vyama vya siasa Mkoa wa Ruvuma wao wamewaomba viongozi ambao wanaenda kinyume na kazi walizotumwa na wananchi kujiudhuru ili kuwapisha viongozi ambao watawatekelezea wananchi mahitaji yao.

hivi jana Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kupangua idara zilizokuwa zikisimamiwa na wizara mbalimbali na kuunda wizara mpya nne visiwani humo.

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Wanachi wa kijiji cha njala matata kilichopo kata ya mkongo wilaya ya namtumbo wamesema tatizo la ukosefu wa maji safi na salama katika kijiji hicho linawathiri kwa kiasi kikubwa wanawake ambao wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta maji .

wamesema kijiji hicho kina vyanzo vingi vya maji lakini vimekuwa vikipekwa maeneo mengine tofauti na maeneo wanayoishi na kuitska serikali kuangali jambo hilo kwa kina kutokana na adha kubwa wanayoipata ya ukosefu maji safi na salama.

wasemema kuwa kutokana na ukosefu huo wa maji kijijni hapo unaweza kusababisha magonjwa ya milipuko na matumbo ya kuhara.



Aug 19, 2013

WAKALI WA SAYARI YETU NA AFRIKA YETU 93.0



Mfaume Pastory na Catherine Shayo ni watangazaji wa kipindi cha AFRIKA YETU ndani ya 93.0 ya Jogoo FM Songea kwani sisi ni wa AFRIKA halisi karibu sana kuisikiliza show yetu kila siku za Juma Pili saa nane kamili mmchana hadi saa kumi kamili jioni.

Lakini ni watangazaji wa kipindi mahiri cha SAYARI YETU cha Jogoo FM ambacho hurushwa kila siku za wiki juma tatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa kumi na mbili kamili jioni........JISIKIE FAHARI, KUISIKILIZA SAYARI .




 WAKALI WA KIPINDI CHA SAYARI NA AFRIKA NA AFRIKA YETU YA 93.0 MOTO CHINI




 TIMU nzima ya kipindi cha AFRIKA YETU ya 93.0 Jogoo Fm kulia Papaa Ramso mutu yenyekujua lighu mingi1!! Ni mtafsri wa nyimbo za kongo anajua lingala, France nk....anafuata ni Catherine shaya Mama wa Afrika yetu na Papaa Mufaume, Paster....Muzee matata wa Afrika yetu......Lakini ni watangazaji wa kipindi mahiri cha SAYARI YETU cha Jogoo FM ambacho hurushwa kila siku za wiki juma tatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa kumi na mbili kamili jioni........JISIKIE FAHARI, KUISIKILIZA SAYARI .



Tuko na mtu wetu anae tuhakikishia usalama wetu bwana


HABARI TOKA RUVUMA TANZANIA


Diwani wa kata ya misufini Salum Mfamaji ambaye pia ni mjumbe wa baraza la katiba manispaa ya songea amewataka wajumbe ambao wanajadili rasimu ya katiba kwa manispaa ya songea kujadili mawazo  ambayo yametolewa na wananchi na sio kwa manufaa ya vyama vyao.

Amesema ni lazima wajumbe ambao wamechaguliwa na wananchi kuwawakilisha wananchi wao kikamilifu badala ya kuangalia maslahi yao binafsi.

Wajumbe wa mabaraza ya mabadiliko ya katiba manispaa ya songea leo wameanza kujadili rasimu iliyopendekezwa na wananchi kwenye mchakato wa kupata maoni ya katiba mjadala ambao utakuwa wa siku tatu kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu matogoro.


Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imeombwa kuanzisha kliniki katika hospitali na vituo vya Afya nchini kwa ajiLi ya walemavu wa ngozi Albino walio athirika na ugonjwa wa saratani ya ngozi ili waathirika hao waweze kutambulika na kupatiwa tiba badala ya kuwapatia dawa za kuzuia mionzi ya jua.

Mwenyekiti wa chama cha Albino nchini Ernest Kimaya ameitaka idara ya ustawi wa jamii kuandaa  bajeti  itakayosaidia Maalbino nchini  kupata huduma ya afya stahiki.

Aidha kimaya amesema kuwa hadi hivi sasa tayari wamesha fanya mazungumzo na wizara na wameanza kutoa dawa ya kuzuia mionzi ya jua katika sehemu mbali mbali nchini.



Wachimbaji wadogo wa madini katika mgodi wa Mererani jijini Arusha  wameitaka serikali kusikiliza madai yao kama wanavyowasikiliza wawekezaji kutoka nje.

Mmoja wa wachimbaji hao wadogo Jackson Manjuu amesema pindi wanapokuwa na mgogoro baina yao na wawekezaji huonekana kuegemewa au kupendelewa zaidi kwa wawekezaji bila kuwajali wachimbaji wadogo ambao ni wazawa.

Manjuu amesema kuwa ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima serikali haina budi kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wazawa.