Jul 22, 2011

KUTOKA ZANZIBAR



1. Makamu w a kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akiangaliwa uharibifu wa mazingira uliotokana na uchimbaji wa matofali karibu na mnara wa Ras Kigomasha Kaskazini Pemba.

2.Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia uharibifu wa mazingira unaotokana na kazi za uchimbaji na upasuaji wa matofali huko kwa Sanani Muwambe, Mkoa wa Kusini Pemba.


Jul 21, 2011

WILAYA YA MJINI

CHAMA CHA WAKULIMA KISIWANI ZANZIBAR,(AFP) KINATARAJIA KUFANYA MATEMBEZI YA HISANI ILI KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUNUNULIA MAFUTA YA KUENDESHEA MAJENERETA 32 YACHAMA HICHO, AMBAYO HUTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA UZALISHAJI.

TAARIFA HAYO IMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MIPANGO SERA NA UENDESHAJI WA CHAMA HICHO, RASHID YUSUPH MCHENGA WAKATI AKIFANYA MAHOJIANO KATIKA KIPINDI CHA SANSETI IN ZANZABAR AMBACHO HURUSHWA NA KITUO HIKI CHA RADIO CHUCHU FM.
YUSUPH MCHENGA, AMEBAINISHA KUWA TATIZO KUBWA LINALOWAKABILIWA WAKULIMA HAPA NCHINI, NI UKOSEFU WA MIKOPO PAMOJA NA PEMBEJEO, AMBAPO AMEIOMBA SERIKALI KUTATUA MATATIZO HAYO ILI KUWAJENGEA UWEZO WAKUZALISHA KARAFUU ILIYO BORA NA KUONGEZA WIGO WA SOKO LA KIMATAIFA.
AIDHA AMEITAKA SERIKALI KUTOWAJENGEA WAKULIMA DHANA YAKUSUBIRI MPAKA WAUZE MAZAO YAO NDIPO WAPATE FEDHA ZA UZALISHAJI.
PIA MKURUGENZI HUYO AMEISHAURI SERIKALI KUSHUSHA USHURU KATIKA VYAKULA VINAVYO INGIA NCHINI ILI KUPUNGA UKALI WA MAISHA KWA WANANCHI.









ZANZIBAR
MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMEWATAKA WANANCHI WA SHEHIYA YA SANANI MUWAMBE KUACHA SHUGHULI ZA UPASUAJI MIAMBA KWA AJILI YA MATOFALI, VINGINEVYO WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

MALIM SEIF AMETOA TAHADHARI HIYO HUKO MUWAMBE ALIKOFIKA KUONA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA SERIKALI, YANAYOWATAKA WANANCHI HAO KUACHANA NA KAZI HIZO ZENYE KULETA UHARIBIFU MKUBWA WA MAZINGIRA, HUKU SERIKALI IKITAFUTA SHUGHULI MBADALA ILI WAWEZE KUJIKIMU NA MAISHA.

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, ILIPIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA UPASUAJI MIAMBA KWA AJILI YA MATOFALI, NA KUITAKA WIZARA YA KAZI, AJIRA NA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI KUTAFUTA SHUGHULI MBADALA KWA WANANCHI HAO, AMBAPO VIKUNDI 18 TAYARI VIMESHASAJILIWA KWA AJILI YA KUPATIWA MIRADI.

AIDHA AMESEMA SERIKALI HAINA NIA YA KUMUONEA MTU YEYOTE, LAKINI IKO MACHO KULINDA SHERIA ZA NCHI NA KUHIFADHI MAZINGIRA YAKE, HIVYO MTU YEYOTE ATAKAEPATIKANA KUHUSIKA NA VITENDO HIVYO ATACHUKULIWA HATUA KALI.

AMEMTAKA MKUU WA WILAYA YA MKOANI KUSHIRIKIANA NA SHEHA WA SHEHIYA HIYO PAMOJA NA WANANCHI KUONA TATIZO HILO LINAONDOKA KABISA KWA MASLAHI YA TAIFA NA KIZAZI CHAO.

KITENDO VYA UPASUAJI WA MIAMBA HIYO KIMETAJWA KKUWA NA ATHARI KUBWA KWA WANANCHI WENYEWE KWA KUZINGATIA MASHIMO HAYO MAKUBWA YAMEZUNGUKA NYUMBA ZAO NA KUHATARISHA MAISHA YA WATOTO WADOGO AU WAGENI WANAOTEMBELEO ENEO HILO.

AIDHA MAALIM SEIF AMESEMA SERIKALI IKO KATIKA HARAKATI ZA KUWATAFUTIA WANANCHI WA KIJIJI HICHO NJIA MBADALA, HIVYO AMELIAGIZA PIA JESHI LA POILISI MKOA WA KASKAZINI PEMBA KUSAIDIA ULINZI KATIKA MAENEO HAYO.








ZANZIBAR

BAADA YA SAKATA LA MIKATABA YENYE UTATA KATIKA BARAZA LA MANISPAA, MEYA WA ZANZIBAR, KHATIB ABRAHMAN KHATIB, AMESEMA HIVI SASA WANAJIANDAA KUONA WATENDAJI WA BARAZA HILO WANATEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZAKE.
AMEYASEMA HAYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, HUKO AFISINI KWAKE MALINDI MJINI ZANZIBAR WALIOFUATILIA UTEKELEZAJI WA RIPOTI YA BARAZA HILO BAADA YA KUANDAA MAPENDEKEZO JUU YA SAKATA LA MIKATABA YENYE UTATA AMBAYO SASA YAPO SERIKALINI KUSUBIRI UAMUZI WAKE.
HIVI KARIBUNI WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WALIISHUPALIA BAJETI YA AFISI YA RAIS IKULU, KWA KULISAKAMA BARAZA HILO JUU YA UTENDAJI KAZI ZAKE NA TUHUMA KUWAPO KWA HARUFU YA RUSHWA ILIYOTEMBEZWA KWA BAADHI YA WATENDAJI AMBAPO WAJUMBE HAO WALITAKA KUJUA MAPENDEKEZO YALIOMO KATIKA RIPOTI HIYO.
MEYA WA MANISPAA HIYO AMESEMA ILI KUWEZA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA TAASISI HIYO HIVI SASA WANACHOKUSUDIA KUKIFANYA NI LAZIMA WATENDAJI WAKUBALI KUONA WANAFUATA SHERIA NA KANUNI ZA BARAZA HILO AMBAPO KILA MFANYAKAZI ATAPASWA KUZIFUATA.
AIDHA AMESEMA TATIZO MBALO LILIBAINIKA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BARAZA HILO KULIKOSEKANA TARATIBU ZA KUFUATA SHERIA KATIKA BAADHI YA MAMBO NA MAAMUZI YALIOKUWA YAKIFANYIKA KIHOLELA.
AMESEMA HIVI SASA TAYARI BARAZA HILO LIMESHAPITISHA BAJETI YAKE AMBAYO INAKUSUDIA KUTUMIA, AMBAYO NI ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 3.7 KWA SHUGHULI ZA BARAZA HILO KWA MWAKA UJAO WA FEDHA WA 2011/2012.








MOROGORO

MAJERUHI WATATU KATI YA 20 WA AJALI YA BASI LA HOOD, ILIYOTOKEA JUZI KATIKA HIFADHI YA WANYAMAPORI MIKUMI, MKOANI MOROGORO WALIOLAZWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA HUO, WANATARAJIWA KUPELEKWA KATIKA TAASISI YA MIFUPA "MOI", PAMOJA NA HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM ILI WAWEZE KUPATIWA MATIBABU ZAIDI BAADA YA HALI ZAO KUONEKANA
KUWA MBAYA.

HAYO YAMEBAINISHWA NA MGANGA MKUU WA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO FRIDA MOKITI, WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI HOSPITALINI HAPO, KUHUSU HALI ZA MAJERUHI HAO.

MGANGA MKUU HUYO AMESEMA KATI YA MAJERUHI HAO MMOJA NI MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA (11), ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JEMIMA ZAMBI HUKU AKISHINDWA KUWATAJA WENGINE, NA KUDAI KUWA BADO MADAKTARI WANAPITA KUKAGUA WAGONGWA NA KWAMBA HUENDA IDADI YAO IKAONGEZEKA.

AIDHA AMESEMA KATI YA HAO WATATU WALIRUHUSIWA, NA KWAMBA HOSPITALI HIYO ILIPOKEA MAJERUHI 41 AMBAPO WENGINE WALIRUHUSIWA NA KUBAKI 21 HUKU WATATU WAMERUHUSIWA LEO.

HATA HIVYO AMESEMA HALI YA MADAWA KATIKA HOSPITALI HIYO SIYO MBAYA, NA KWAMBA WALIPATA MSAADA WA BAADHI YA MADAWA YALIYOPUNGUA KUTOKA KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JITU PATEL.

KWA UPANDE WAKE MMILIKI WA KAMPUNI YA MABASI YA HOOD, MOHAMED HOOD AMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA AJALI HIYO NA KUAHIDI KUTOA MSAADA KWA NDUGU WA MAREHEMU WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI HIYO PAMOJA NA KUWASAIDIA MAJERUHI.

Jul 20, 2011

ZANZIBAR

SHIRIKA LA BANDARI NA IDARA YA MAZINGIRA ZANZIBAR, IMETAKIWA KUWASILISHA TAARIFA YA KITAALAMU, KWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, JUU YA ATHARI ZA KIMAZINGIRA NA ZA KIMAAFA ZINAZOWEZA KUPATIKANA, KUTOKANA NA UJENZI WA HOTELI YA KITALII KARIBU NA BANDARI YA WESHA, KATIKA KIPINDI KISICHOZIDI WIKI SITA.

MAALIM SEIF AMETOA AGIZO HILO LEO WAKATI AKIFANYA MAJADILIANO MAFUPI NA VIONGOZI WA TAASISI HIZO PAMOJA NA MENEJIMENT YA HOTELI YA KITALII YA PEMBA MISALI COTTAGE, KATIKA OFISI ZA BANDARI HUKO WESHA.

AMESEMA UJENZI WA HOTELI YA KITALII YA ‘PEMBA MISALI COTTAGE’ ILIOAMBATANA NA ‘JET’ NA KUEZEKWA KWA MAKUTI WASTANI WA MITA 20 TU KUTOKA YALIPO MATANGI YA MAFUTA YA GAPCO YENYE UWEZO WA KUHIFADHI TANI 1000, NI HATARI KWA MAISHA YA BINAADAMU WAISHIO HOTELINI HAPO NA WALE WALIOKO MAENEO YOTE JIRANI.

AIDHA AMESEMA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, ITAENDELEA KUENDESHA SHUGHULI ZAKE KWA KUZINGATIA KANUNI NA SHERIA ZILIZOPO BILA YA KUMPENDELEA AU KUMUONEA MTU.

AMEZITAKA TAASISI HIZO KUKAA PAMOJA NA KUFANYA UKAGUZI WA KINA NA HATIMAE KUTAYARISHA TAARIFA ZA KITAALAMU BAADA YA IDARA YA MAZINGIRA KUANDAA HADIDU REJEA.

KATIKA KIKAO HICHO, IMEAFIKIWA MMILIKI WA HOTELI YA PEMBA MISALI COTTAGE KUGHARAMIA GHARAMA ZA UTAFITI WA KITAALAMU UTAKAOFANYIKA.

AIDHA MAALIM SEIF ALIPATA FURSA YA KUTEMBELEA BANDARI ZA WETE NA WESHA PAMOJA NA KUANGALIA MNARA WA KUONGOZEA MELI WA RAS KIGOMASHA, SAMBAMBA NA KUIKAGUA NYUMBA YA WAGENI YA’BOMAN GUEST HOUSE’ INAYOMILIKIWA NA SHIRIKA HILO.

SINGIDA

TAASISI YA KUZIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU) MKOA WA SINGIDA IMEPOKEA JUMLA TAARIFA 476 ZA TUHUMA ZA MATUKIO YA VITENDO VYA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA KATIKA KIPINDI CHA KUANZIA MWAKA 2005 HADI MWAKA HUU.

MKUU WA TAKUKURU MKOANI SINGIDA,BI JULLIANE KALLASSA AMEYASEMA HAYO LEO KATIKA SEMINA YA SIKU MOJA KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI WANAOFUNDISHA SOMO LA URAIA KATIKA SHULE ZA MKOA HUO WAKATI AKITOA HALI HALISI YA MATUKIO YALIYOPOKELEWA NA TAASISI HIYO KATIKA KIPINDI HICHO.

KWA MUJIBU WA BI. KALLASSA, KATI YA TAARIFA HIZO ZINAZOHUSU VITENDO VYA RUSHWA NI 367 WAKATI TAARIFA ZINAZOHUSU MASUALA YA UCHAGUZI NI 11 NA TAARIFA 16 KESI ZAKE ZIPO MAHAKAMANI HUKU KUKIWA NA MAJALADA MAWILI YANAHUSU TUHUMA ZA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA ULIOPITA.

AIDHA MKUU HUYO WA TAASISI YA KUZIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA HAKUWA TAYARI KUWEKA BAYANA MAJINA YA WATUHUMIWA PAMOJA NA TUHUMA ZILIZOPELEKWA KWA MWANDESDHA MASHTAKA MKUU WA SERIKALI.

HATA HIVYO HABARI AMBAZO BADO HAZIJATHIBITISHWA NA MSEMAJI HUYO ZINASEMA KWAMBA MAJALADA MAWILI YALIYOPO KWA DPP YANAWAHUSISHA WALIOKUWA WABUNGE WA MAJIMBO YA IRAMBA MASHARIKI NA IRAMBA MAGHARIBI (CCM) WALIOKUWA WAKIKABILIWA NA TUHUMA ZA KUPOKEA POSHO ZA VIKAO LICHA YA KUTOHUDHURIA KWENYE VIKAO HUSIKA VYA HALMASHAURI HIYO.

KWA MUJIBU WA HABARI HIZO TUHUMA AMBAZO BADO ZINAFANYIWA UCHUNGUZI NA TAASISI HIYO ZIMEWATAJA WALIOKUWA WAGOMBEA UBUNGE KATIKA MAJIMBO MAWILI YALIYOPO MKOANI SINGIDA YALIYOGOMBEWA NA WATU MAARUFU NA WENYE UWEZO WA KIFEDHA AMBAO HAWAKUTAJWA MAJINA.

SEMINA HIYO YA SIKU MOJA ILIANDALIWA NA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA ILIJUMUISHA WASHIRIKISHA 25 AMBAO NI WALIMU WANAOFUNDISHA SOMO LA URAIA KUTOKA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA MKOA WA SINGIDA,KATIKA WILAYA ZA IRAMBA,MANYONI,SINGIDA VIJIJINI NA MANISPAA YA SINGIDA.

DAR ES SALAAM

SHEIKH MKUU WA TANZANIA MUFTI SHAABAN BIN SIMBA, AMEITAKA JAMII NCHINI KUTAMBUA NA KUTHAMINI MICHANGO YA WALEZI NA WANAHARAKATI WANAOJITOLEA KULEA WATOTO YATIMA NA WALE WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

AMEYASEMA HAYO WAKATI WA MAHAFALI YA CHUO CHA SALAFINA ISLAMIC CENTRE KILICHOPO BUNJU NJE KIDOGO YA JIJI LA DAR ES SALAAM, AMBAPO AMESEMA UMEFIKA WAKATI KWA WAISLAMU KUTHAMINI HARAKATI HIZO KWA KUWAUNGA MKONO KWA VITENDO WALEZI HAO.

AMESEMA NI VEMA MATAJIRI WA KIISLAMU NA MSIOKUWA WAISLAMU KUJITOKEZA KUUNGA MKONO JITIHADA HIZO LI KUWAJENGEA UWEZO WA WAKUTIMIZA MALENGO NA MAAGIZO YA ALLAH (SW) NA MTUME WAKE.

AIDHA MUFTI SIMBA PAMOJA NA MWENYEKITI WA SIC, SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIR, WAMETOA SHUKRANI ZA PEKEE KWA MFADHILI WA CHUO HICHO, ABDUL ZAKARIA KWA KUWEZESHA UJENZI WA MAJENGO YA KISASA KWA MASLAHI YA DINI NA JAMII YA WATANZANIA KWA UJUMLA.

KUTOKANA NA HATUA HIYO MUFTI, AMETOA WITO NA KUWAOMBA MATAJIRI WA KIISLAMU NDANI NA NJE YA NCHI KUCHANGIA KUKIENDELEZA KIPATE MAJENGO ZAIDI KWA AJILI YA VITIVO MBALIMBALI VITAKAVYOTUMIKA KUWAJENGA VIJANA KIDUNIA NA KIAKHERA.

KWA UPANDE WAKE MWENYEKITI MTENDAJI WA TAASISI HIYO SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIR AMESEMA KUWA MAADHIMISHO YA MAHAFALI HAYO YA 12 YALIANZA TOKA MWAKA 1999 AMBAPO HADI SASA ZAIDI YA WANAFUNZI 600 WAMEHITIMU ELIMU YAO AMBAPO HIVI SASA WANAFANYAKAZI KATIKA TAASISI MBALIMBALI NCHINI.

Jul 19, 2011

ZANZIBAR

WIZARA YA MIUNDO MBINU NA MAWASILIANO IMESEMA HAITOWEZA KUZITEKELEZA AHADI ZILIZOTOLEWA NA MARAIS WALIOONDOKA MADARAKANI ZA KUZIFANYIA MATENGENEZO BARABARA ZA NDANI KWA WAKATI MMOJA NA BADALA YAKE ITAFANYA KAZI HIYO HATUA KWA HATUA.

NAIBU WAZIRI WA WIZARA HIYO, ISSA HAJI USSI AMETOA UFAFANUZI HUO BARAZANI HII LEO WAKATI AKIJIBU SUALI LA MWAKILISHI WA KWAMTIPURA HAMZA HASSAN JUMA.

MWAKILISAHI HUYO ALITAKA KUJUA LINI SERIKALI ITATEKELEZA AHADI ZA MARAIS WALIOPITA KATIKA KUZIFANYIA MATENGEZO BARABARA ZA NDANI IKIWEMO YA MBORIBORINI.

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MIUNDOMBINU AMEKIRI KUWEPO AHADI HIZO NA KUSEMA ZINATHAMINIWA NA KUHESHIMIWA NA WIZARA YAKE INAZIHESHIMU, LAKINI ZINASHINDWA KUTIMIZWA KWA WAKATI MMOJA.

AMESEMA WIZARA HIYO ITAHAKIKISHA KUWA INALIONDOA TATIZO HILO KILA PALE ITAPOKUWA INAPATA UWEZO KWANI HIVI SASA WAMEANZA KUPUNGUZA MOJA BAADA NYENGINE.

AIDHA AMEWATAKA WANANCHI WASIVUNJIKE MOYO KUTOKANA NA WIZARA HIYO KUZIFANYIAKAZI AHADI ZOTE ZA UJENZI WA BARABARA INAYOANZIA KWA ABASI HUSSEIN KUPITIA MBORIBORINI HADI AMANI DARAJA BOVU.

ZANZIBAR

BAADHI YA WAWAKILISHI WA BARAZA LA SERIKALKI YA MAPINDUZI ZANZIBAR, WAMETOA WITO KWA WIZARA YA KAZI UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NA USHIRIKA, KUANDAA MPANGO UTAKAOTOA ELIMU KWA VIJANA ITAKAYO WAWEZESHA KUJIARI, NA KUWAPATIA MIKOPO ITAKAYO WASAIDIA KUANZISHA MIRADI YAO.

WITO HUO UMETOLEWA LEO NA WAWAKILISHI KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA WAWAKILISHI, WAKATI WAKICHANGIA HOJA ZAO JUU YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA KAZI UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NA USHIRIKA.

AKIZUNGUMZA KATIKA BARAZA HILO MWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI SALMIN AWARI, AMEBAINISHA KUA TATIZO KUBWA LINALOWAKABILI VIJANA NI UKOSEFU WA AJIRA AMBAPO AMESEMA LINATOKANA NA DHANA KUWA, VIJANA WENGI WANASHINDWA KUJIAJIRI.

SERIKALI KWA UPANDE WAKE INASEMA HAINA UWEZO WA KUAJIRI WATU WOTE, HIVYO NI VYEMA KWA SASA WANACHI WAELEKEZE NGUVU ZAO KATIKA KUJIAJIRI WENYEWE.

PAMOJA NA KAULI HIYO YA SERIKALI, ELIMU IMETAJWA KUWA MSINGI MUHIMU KATIKA KUWAJENGEA VIJANA UWEZO WAKUJIAJIRI HIVYO SERIKALI IMESHAURIWA PIA KUSHIRIKIANA KIKAMILIFU NA TAASISI ZINAZOHUSIKA KATIKA KUWAWEZESHA VIJANA ILI KUTATUA TATIZO HILO.

AIDHA WAWAKILISHI WAMEITAKA SERIKALI NA WIZARA HUSIKA KUWEKA WAZI SIFA ZITAKAZO MWEZESHA MWANANCHI KUPATA MKOPO ILI WANANCHI WAPATE KUZIFAHAMU.

IMEBAINISHWA KUWA ENDAPO SERIKALI ITAAMUA KUIWEZESHA SEKTA YA AJIRA, BASI TATIZO LA AJIRA NA UMASIKINI LITAONDOKA MIONGONI MWA WANANCHI WAKE.

ZANZIBAR

SERIKALI YA ZANZIBAR IMESEMA KUWA INASHINDWA KUIRUHUSU HOSPITALI INAYOMILIKIWA NA JESHI LA WANANCHI KATIKA KIJIJI CHA WAWI KISIWANI PEMBA, KUTOA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA UKIMWI ARV KUTOKANA NA KUKOSA SIFA YA WAHUDUMU MAALUM WA KUDUMU KATIKA HOSPITALI HIYO.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, SIRA UBWA MAMBOYA, AMETOAUFAFANUZI HUO KUFUATIA SUALI ALILOULIZWA BARAZANI NA MWAKILISHI WA JIMBO HILO, SALEH NASSOR.

MWAKILISHI HAYO AMETAKA KUJUA KWANINI HOSPITALI HIYO HAIRUHUSIWI KUTOA DAWA ZA ARV INGAWA IMETENGENEZWA KWA MFUMO WA KISASA.

NAIBU WAZIRI HUYO AMESEMA WIZARA YAKE INASHINDWA KUWEKA DAWA HIZO KATIKA KITUO HICHO KWA VILE HAKUNA DAKTARI AMBAYE ATAWEZA KUKAA MUDA WOTE JAMBO AMBALO LINAIFANYA WIZARA HIYO KUSHINDWA KURUHUSU UTOAJI WA DAWA HIZO KATIKA HOSPITALI HIYO.

AIDHA AMESEMA HALI HIYO WANALAZIMIKA KUSHINDWA KWA KUFANYA HIVYO KUTOKANA NA KAZI AMBAZO ZINAHITAJIKA KUFANYIKA WAKATI WA UTOAJI DAWA HIZO HULAZIMIKA KUTOLEWA USHAURI JAMBO AMBALO LITAKOSEKANA IKIWA HAKUNA DAKTARI KWA MUDA WOTE.

AMESEMA DAWA ZA ARV, ZIMEAMUALIWA KUTOLEWA KATIKA VITUO MAALUM IKIWA NI HATUA YA WIZARA HIYO KUWEKA UTARATIBU MZURI WA UTOAJI DAWA HIZO KATIKA HOSPITALI ZA SERIKALI.

AMESEMA IKIWA HOSPITALI YA WAWI ITAWEZA KUPATA DAKTARI ATAESIMAMIA UTOAJI WA DAWA HIZO, WIZARA HIYO HAITASITA KUFANYA HIVYO KWANI DHAMIRA YA SERIKALI KUHAKIKISHA KUNAKUWA NA UTARATIBU MZURI WA AFYA.

ZANZIBAR

SERIKALI INAHITAJI SHILINGI BILIONI 120 KUONDOA TATIZO LA UPATIKANAJI MAJI SAFI NA SALAMA KATIKA MKOA WA MJINI MAGHARIBI.

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAKAAZI, ARDHI, MAJI NA NISHATI HAJI MWADINI MAKAME AMEYASEMA HAYO LEO WAKATI AKIJIBU SUALI LA NYONGEZA LA MWAKILISHI WA VITI MAALUM VIWE KHAMIS ABDALLA, ALIYETAKA KUJUA LINI TATIZO LA MAJI KATIKA MAENEO HAYO LITAMALIZIKA.

NAIBU WAZIRI AMESEMA NI KWELI TATIZO LA MAJI KATIKA MAENEO YA MJINI NI KUBWA KIASI AMBACHO SERIKALI ITAHITAJI KUWA NA SHILINGI BILIONI 120 ILI KUWEZA KUKABILIANA NA TATIZO HILO NA KUMALIZIKA KABISA.

AMESEMA KUTOKANA NA HALI HIYO, WIZARA YAKE IMEAMUA KUTENGA SHILINGI MILIONI 40 NDANI YA KIPINDI CHA MIAKA MITATU KUWEZA KUONDOA TATIZO HILO KWA UNGUJA NA PEMBA.

AKITA SABABU ZILIZOPELEKEA HALI HIYO NIPAMOJA NA BAADHI YA WANANCHI KUJENGA MAHODHI MAKUBWA CHINI YA ARDHI YANAYOSABABISHA SEHEMU KUBWA YAHUDUMA HIYO KUTUMIWA NA WATU WACHACHE.

AMEBAINI TATIZO JINGINE TATIZO JENGINE NI UCHAKAVU WA MIUNDO MBINU YA USAMBAZAJI WA HUDUMA YA MAJI NA UJENZI HOLELA UNAOFANYIKA KATIKA VYANZO VYA MAJI NA MTANDAO WA MAJI HUKU MAHODHI YALIOJENGWA YAKIWA HAYAKO KITAALAMU.

WILAYA YA MJINI

WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO WAMEIOMBA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, KUWAWEZESHA KWA KUWAPATIA MIKOPO AMBAYO ITAWASAIDIA KUJIENDELEZA KIMAISHA.

HAYO YAMEELEZWA NA MFANYABIASHARA MMOJA, MUSSA NASSOR OMAR WAKATI AKIZUNGUMZA NA CHUCHU FM HAPO OFISINI KWAKE MICHEZANI MJINI UNGUJA.

AIDHA MUSSA AMESEMA IWAPO SERIKALI ITAWAWEZESHA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO KWA KUWAPATIA MIKOPO MBALINBALI, WATAWEZA KUONDOKANA NA HALI YA UTEGEMEZI, PAMOJA NA KUKAA MASKANI NA KUWEZA KUEPUKANA NA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA.

MUSSA AMESEMA ANAJISHUGHULISHA NA KAZI YA USHONAJI WA VIATU AMBAYO KAZI YAKE HIYO, IMEKUWA IKIMPATIA KIPATO KIASI AMBACHO AMEWEZA KUJIKIMU KIMAISHA PAMOJA NA KUWASOMESHA WATOTO WAKE.

SAMBAMBA NA HAYO AMEWATAKA VIJANA KUJISHUGHULISHA NA KAZI MBALIMBALI, AMBAZO ZITAWEZA KUWAPATIA AJIRA NA KUWACHA KUTEGEMEA AJIRA KUTOKA SERIKALINI.

Jul 18, 2011

JOMBAAZ KUTOKA CHUCHU FM RADIO ZANZIBAR


KUTOKA KUSHOTO NI ISSA NDOKEJI, HALIFA MMANGA(RAS MIDUDE) NA MFAUME PASTORY(MKALI WA X-CLUSIVE)

CHEKI NA HIZO BASI

ZANZIBAR

KATIKA KUKABILIANA NA BAADHI YA MICHANGO ISIYOKUWA YA LAZIMA AMBAYO IMEKUA IKITOZWA MASHULENI, WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR, INAJIANDAA KUUNDA MUUNDO MAALUM, UTAKAO TOA MWONGOZO JUU YA KAZI ZA UCHANGIAJI WA WIZARA HIYO.

HAYO YAMEELEZWA HII LEO NA NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI, ZAHRA ALI HAMAD, WAKATI AKIJIBU HOJA MBALIMBALI ZILIZO ELEKEZWA KATIKA WIZARA YAKE NA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI.

MUONGOZO HUO UNAKUJA BAADA YA KUSIKIKA KWA KILIO CHA WANAFUNZI,KUWA WAMEKUA WAKIKATAZWA NA WALIMU KUENDELEA NA MASOMO KWA SABABU ZA KUSHINDWA KULIPIA FEDHA ZA MICHANGO YA ELIMU.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU AMEBAINISHA KUA MICHANGO WANAYOPASWA KUTOZWA WAZAZI NA WALEZI WA WANAFUNZI, NI ILE TU AMBAYO IMEPITISHWA NA WIZARA YA ELIMU, KAMA KUCHANGIA SIKU YA WALIMU DUNIANI NA MICHANGO YA MWENGE AMBAYO HAITAKIWI KUZIDI SHILINGI ELFU TANO.

AIDHA WAZIRI AMEWATA WAZAZI KUTAMBUA KUWA KUCHANGIA MAENDELEO YA SHULE NI WAJIBU WAO, HIVYO NIVYEMA WAKAWA WEPESI KATIKA KUCHANGIA MICHANGO INAYOKUBALIKA KISHERIA, ILI KUHAKIKISHA WATOTO WANAPATIWA ELIMU ILIYOBORA.

AKIZUNGUMZIA TATIZO LA UHABA WA WALIMU NAIBU WAZIRI WA ELIMU AMESEMA, WIZARA ITAJITAHIDI KUZIBA MAPUNGUFU YALIYOPO.

PIA AMEISHAURI WIZARA KUPITIA KUVIPITIA VYUO VYA KURAANI NA MADRASA ILI IWEZE KUVIPATIA NYENZO ZA KUFUNDISHIA IKIWA KWA SASA WANATEGEMEA KUTAFUTA VIFAA HIVYO KUPITIA WAHISANI MBALIBALI.

WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA

WANANCHI WA SHEHIYA YA MAUNGANI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA, WANAIOMBA KAMPUNI YA MTANDAO WA MAWASILIANO YA SIMU ZA MKONONI YA ZANTEL, KUFANYA JUHUDI YA KUWAEKEA MNARA KATIKA SHEHIYA YAO ILI KUWEZA KUPATA MAWASILIANO MAZURI.

HAYO YAMEBAINIKA WAKATI CHUCHU FM ILIPOFIKA KATIKA SHEHIYA HIYO, NA WANANCHI HAO WAMESEMA KWA MUDA MREFU WAMEKUWA WANAKABILIWA NA TATIZO LA MAWASILIANO YA ZANTELI HALI AMBAYO IMEKUWA INAWAPA USUMBUFU MKUBWA.

NAE SHEHA WA SHIYA HIYO ALI KIBWANA JUMA, AMESEMA NI KWELI TATIZO HILO LIPO NA TAYARI AMESHAPELEKA MALALAMIKO KWA KAMPUNI HIYO, LAKINI HADI SASA BADO HAKUNA HATUWA ZOZOTE ZILIZOCHUKULIWA.

AIDHA SHEHA HUYO AMESEMA WAKATI MWENGINE HUTOKEA MATATIZO MBALIMBALI YAKIWEMO UHALIFU, LAKINI HUSHINDWA KUTOWA TAARIFA ZA HARAKA KATIKA SEHEMU HUSIKA KUTOKANA NA UGUMU WA MAWASILIANO HAYO.

HATA HIVYO SHEHA HUYO AMESEMA WAO WAPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI HIYO,ILI KUHAKIKISHA KUWA TATIZO HILO LINAONDOKA NA KUWEZA KUPATA MAWASILIANO MAZURI KAMA WAVYOPATA WAKAAZI WA SHERIYA NYENGINE.

DODOMA

MJADALA WA BAJETI YA WIZARA MUHIMU KWA MAENDELEA YA TAIFA YA NISHATI NA MADINI, UNATARAJIWA KUMALIZIKA USIKU HUU, AMBAPO WAZIRI WILIAM NGELEJA AMESHAURIWA KUTAFUTA SULUHISHO LA KUDUMU KATIKA KUONDOKANA NA TATIZO LA MGAO UMEME.

PAMOJA NA KUELEKEA KUMALIZIKA KWA MJADALA WA BAJETI HIYO, KUNAHATI HATI KUBWA YA KUTOPITISHWA KWA KWAKE KUTOKA NA WABUNGE KUONEKANA KUTORIDHIKA NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI WIZARA HIYO.

WABUNGE WALIOWENGI WAMEBAINISHA VIPENGELE MUHIMU AMBAVYO VIMETAJWA KUWA SABABU ZA KUTOPITISHWA KWA BAJETI HIYO, KUWA NI TATTIZO LA MGAO WA UMEME,WIZI WA MADINI NA MIKATABA MIBOVU PAMOJA NA ENEO LA GESI NA MAFUTA, MAENEO AMBAYO WAMEIUTAKA SERIKALI KUYAFANYIA MABADIRIKO YA MIKATABA.

AIDHA WABUNGE WAMEILAUMU SERIKALI KUWA HAIWAPI WANANCHI KIPAUMBELE KATIKA KUNUFAIKA NA MAENEO YA ARDHI ZAO BADALA YAKE IMEKUA IKIRUHUSU WATAFI KUJA NA WATAALAM PAMOJA NA WAFANYAKAZI NJE NAKUWAPATIA AJIRA HUKU WAZAWA WAKIBAKI BILA AJIRA.

KATIKA KUKABIULIANA NA CHANGAMOTO ZOTE HIZO SERIKALI IMESHAURIWA KUTOTAPA KIGUGUMIZI KATIKA KUSIMAMIA NA KUTEKELEZA SHERIA ZA NCHI, AMBAPO WIZARA YANISHATI NA MADINI IMTAKIWA KUACHANA NA MITAMBO YA KUKODI BADALA YAKE ITAFUTE MITAMBO IMARA NA YAKUDUMU.

MJADALA WABAJETI WA BAJETI HII, NIMIONGONI MWA MIJADALA MIKUU ILIYOKUWA IKISUBIRIWA KWA HAMU NA WANANCHI, AMBAPO MPAKA UNAKWENDA KUMALIZIKA WABUNGE WAMEONEKANA KUMUWEKA KATIKA WAKATI MGUMU WAZIRI WA WIZARA HIYO WAILAM NGELEJA.

UNAENDELEA KUSIKILIZA TAARIFA YA HABARI KUTOKA HAPA CHUCHU FM 
 

ZIFUATAZO SASA NI HABARI ZA KIMATAIFA.

TRIPOLI

MAPAMBANO MAKALI KUUWANIA MJI WENYE UTAJIRI WA MAFUTA WA BREGA BADO YANAENDELEA NCHINI LIBYA.

MSEMAJI WA WAASI WA LIBYA, MOHAMMED ZAWI, AMESEMA LICHA YA WAO KUFANIKIWA KUINGIA KATIKA MJI HUO, BADO HAWAJAFANIKIWA KUUDHIBITI WOTE KUTOKA KWA WANAJESHI WA GADDAFI.

TANGU MAPIGANO KUUPIGANI MJI HUO YAANZE ALHAMISI ILIYOPITA, JUMLA YA WAPIGANAJI 15 WAMEUAWA NA WENGINE 274 WAMEJERUHIWA.

WAKATI MAPIGANO MAKALI YAKIENDELEA KATIKA MJI HUO WA BREGA, MFULULIZO WA MIRIPUKO IMEUPIGA MJI MKUU WA LIBYA, TRIPOLI, BAADA YA KIONGOZI WA NCHI HIYO MUAMMAR GADDAFI KUAPA KWAMBA KAMWE HATAJIUZULU NA KUKIMBILIA UHAMISHONI.

WAKATI HUO HUO, URUSI LEO IMEIKOSOA MAREKANI NA NCHI NYINGINE KWA KULITAMBUA BARAZA LA MPITO LA WAASI WA LIBYA KAMA SERIKALI HALALI KWA KUSEMA KWAMBA NI KUEGEMEA UPANDE MMOJA KATIKA VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE.

CAP TOWN

RAIS OBAMA AMESEMA MANDELA NI NEMBO YA DEMOKRASIA DUNIANI

NELSON MANDELA AMBAYE KWA SASA NI MYONGE KIAFYA AMEKUWA CHINI YA UANAGILIZI WA KARIBU KUTOKA KWA MADAKATARI KWA MUDA WA SAA 24 TANGU ATOKE HOSPITALI MWEZI JANUARI PALE ALIPOLAZWA BAADA YA KUUGUA.

LAKINI HALI HII HAIJAWAZUIA RAIA WA AFRIKA KUSINI NA WATU WENGI DUNIANI KUMTAKIA KHERI NJEMA ANAVYO SHEHEREKEA MIAKA 93 TANGU AZALIWE.

KATIKA KUADHIMISHA SIKU HII, NYIMBO MAALUM IMETUNGWA KWA HESHIMA YAKE, RAIA WA AFRIKA KUSINI WAMEWEKA HISTORIA AMBAPO YAMKINI WATU MILIONI 12 WAMEIMBA WIMBO HUO KWA WAKATI MMOJA.

SHIRIKA LA UTANGAZAJI NCHINI HUMO (SABC) PAMOJA NA IDARA YA ELIMU WAMEFANYA MPANGO KUWA ILIPOTIMU SAA MBILI NA DAKIKA ASUBUHI, WANAFAUNZI KATIKA SHULE ZOTE NCHINI HUMO WALIIMBA WIMBO HUO MAALUM ULIOTUNGWA KWA HESHIMA YA MADIBA.

SIKU HII YA KUZALIWA KWA NELSON MANDELA, RAIS WA KWANZA MWEUSI WA AFRIKA KUSINI NI SIKU YA KIMATAIFA ILIORODHESHWA NA UMOJA WA MATAIFA.

NCHINI AFRIKA KUSINI HII LEO KILA MTU AMEJITOLEA DAKIKA 67 ZA MUDA WAKE WA KUFANYA HUDUMA ZA KIJAMII.

VIONGOZI MBALI MBALI DUNIANI WAMEMTUMIA SALAMU ZA KHERI NJEMA MZEE MANDELA WAKIONGOZWA NA RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI.

RAIS OBAMA AMESEMA MANDELA NI NEMBO YA DEMOKRASIA NA HAKI DUNIANI NA AMEMSHUKURU KWA KUJITOLEA MAISHA YAKE KWA HUDUMA YA JAMII.

KIONGOZI HUYO WA MAREKANI AMESEMA MANDELA ATAACHA URITHI WA BUSARA, NGUVU NA FADHILA NYINGI.

Jul 17, 2011

ZANZIBAR

VIJANA NCHINI WAMETAKIWA KUWA TAYARI KUFANYA KAZI ZA KUJITOLEA ZENYE MANUFAA KWAO NA TAIFA.

HAYO YAMEELEZWA LEO NA MAKAMU WA PILI WA RAIS, BALOZI SEIF ALI IDDI,WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI ENDELEVU YA USAFI WA MAZINGIRA ILIYOANDALIWA NA JUMUIYA ISIYO YA KISERIKALI YA ZASOSE KATIKA UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZAMANI MNAZI MMOJA.

BALOZI SEIF AMESEMA VIJANA WANAPASWA KUFAHAMU KWAMBA WAZANZIBARI NA WATANZANIA LAZIMA WAFANYEKAZI WENYEWE NA KUACHA TABIA YA UTEGEMEZI.

BALOZI SEIF AMETOA HISTORIA YA KUFANYA KAZI ZA KUJITOLEA ILIFANYIKA MIAKA MINGI NA KUWEZA KUJIPATIA UMAARUFU NI PAMOJA NA UJENZI WA NYUMBA ZA MAENDELEO,UNGUJA NA PEMBA,UJENZI WA UWANJA WA AMAAN,UJENZI WA BARABARA MBALI MBALI,SKULI NA MAMBO MBALI AMBAYO YAMEWEZA KULETA MAENDELEO MAKUBWA YA NCHI.

AMEWATAKA VIJANA KUFAHAMU KUA HAKUNA SHUGHULI ZA MAENDELEO ZILIZOFANYIKA KISIWANI ZANZIBAR BILA YA NGUVU ZA VIJANA AMBAPO KWA PAMOJA WALIAMUA KUJITOLEA.

AIDHA BALOZI SEIF AMEPONGEZA VIJANA NA HASA JUMUIYA YA ZASOSE KWA KUFANYA UAMUZI WA KUANZISHA KAMPENI YA USAFI UNAOTOKANA NA KUGUSWA NA TAMKO LA RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMMED SHEIN LILILOSEMA KUWA HALI YA MJI WA ZANZIBAR HAIRIDHISHI.

KWA UPANDE WAKE KATIBU MTENDAJI WA JUMUIYA HIYO, SHAKA HAMDU SHAKA AMESEMA KUWA LENGO KUU LA KUANZISHA JUMUIYA HIYO NI KUSIMAMIA,KUHAKIKISHA NA KUTOA MUAMKO KWA VIJANA NA JAMII JUU YA SUALA LA USAFI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA.

KATIKA UZINDUZI HUO, JUMLA YA SHILINGI MILIONI 2,600,000 ZIMEKUSANYWA KWA AJILI YA KUCHANGIA JUMIYA HIYO HUKU AMBAPO WENGINE WAMEAHIDI KUTOA JUMLA YA SHILINGI MILIONI 5,555,000 TANO LAKI TANO NA HAMSINI ELF.

ZANZIBAR

WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NA USHIRIKA IMESEMA ITAENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WA ELIMU WANAUSHIRIKA NA WAJASIRIAMALI WENGINE KAMA MBINU YA KUWAPA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WA KUZALISHA BIDHAA BORA NA KUKUZA FURSA ZA AJIRA.

AKITOA MAELEKEZO KWA WAJASRIAMALI WALIOKUWA WAKIJIANDAA KWENDA MWANZA KWA MAFUNZO YA UJASIAMALI, KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO, ASHA ALI ABDULLA AMESEMA SERIKALI ITAFIKIA LENGO HILO KWA WATU WENGI ZAIDI.

AIDHA AMESEMA KATIKA KIPINDI AMBACHO NI CHA USHINDANI WA KIBISHARA NA HUDUMA WAJASIRIAMALI ZANZIBAR LAZIMA WABADILIKE NA KUTEGENEZA BIDHAA ZITAKAZOMUDU USHINDANI KATIKAMASOKO YA KIBIASHARA NCHINI

WAJASIRIAMALI WANAOHUDHURIA MAFUNZO YA MATUMIZI YA NGOZI KUTENGENEZA VIATU AINA YA KUBADHI KUTOKA PEMBA NA UNGUJA WAMETAKIWA KUWA MAKINI KATIKA MAFUNZO HAYO NA KUCHUKUA ELIMU ILI WATAKAPORUDI NYUMBANI WAWE WALIMU KWA WENZAO.

ZIARA HIYO IMEGHARAMIWA NA SERIKALI KUPITIA WIZARA KAZI NA UWEZESHAJI KWA KUSHIRIKIANA NA WAWAKILISHI WA MAJIMBO YA KIKWAJUNI NA WAWI PEMBA.

KWA UPANDE WAKE KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO, ALI JUMA AMESEMA INASHANGAZA KUONA BIDHAA NYINGI ZINAZOTOKANA NA SANAA ZA MIKONO KATIKA MJI WA ZANZIBAR HAZITOKI ZANZIBAR.

AMESEMA BIDHAA NYINGI NA SANAA ZINATOKA NJE YA ZANZIBAR HIVYO HAZIONESHI UTAMADUNI HALISI WA ZANZIBAR AMBAPO AMEWATA WAJASIRIAMALI KUWA WABUNIFU ZAIDI ILI KULETA USHINDANI KIBIASHARA.

WILAYA YA MJINI MAGHARIBI

KATIBU MTENDAJI JUMUIYA YA KUHIFADHI MAZINGIRA RAS FUMBA (FUPECO), ABDULRAZAK SHAABAN JUMA, AMESEMA LENGO LA KUANZISHWA JUMUIYA HIYO NI KUHIFADHI MAZINGIRA YA BAHARINI NA NCHI KAVU ILI KULETA MAENDELEO ENDELEVU NA USTAWI WA WANAJAMII WA FUMBA.

AMEYASEMA HAYO HII LEO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUMALIZIKA KAMPENI YA USAFI KATIKA MAENEO YA FUKWE YA BAHARI YA KORORO ILIYOPO FUMBA, WILAYA YA MAGHARIBI.

JUMUIYA HIYO IMEAMUA KUFANYA USAFI KATIKA MAENEO YA FUKWE HIYO KUTOKANA NA MAZINGIRA YAKE KUWA KATIKA HALI MBAYA INAYOWEZA KULETEA ATHARI KWA VIUMBE WA BAHARINI NA NCHI KAVU.

JUMA AMEELEZA KUWA JUMUIYA HIYO IMEANZA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ILI KUREJESHA MANDHARI YA ASILI KATIKA FUKWE HIYO ILI KUWEZE KUPATIKANA KWA MAENDELEO YA ZANZIBAR.

AIDHA AMESEMA MAZINGIRA YA BAHARI HIYO YAMEATHIRIWA VIBAYA NA UTUPAJI TAKA, MIFUKO YA PLASTIKI, UCHIMBAJI MCHANGA NA UKATAJI MITI OVYO KWA AJILI YA KUTENGENEZA MAKAA.

AKIZUNGUMZIA CHANGAMOTO ZA JUMUIYA HIYO, AMESEMA NI PAMOJA NA UKOSEFU WA VITENDEA KAZI KAMA MAPANGA VIATU MAALUM, MABARO GLAVU KUZUIA UCHAFU NA VIFAA VYENGINE VIDOGO VIDOGO.

HIVYO, AMEWATAKA WAFADHILI MBALI MBALI KUJITOKEZA KATIKA KUIUNGA MKONO JUMUIYA HIYO AMBAYO BADO NI CHANGA ILI IWEZE KUFANYA KAZI ZAKE KWA UFANISI ZAIDI.

JULY 7 ITS MY BIRTHDAY

TAREHE SABA MWEZI WA SABA NISIKU AMBAYO NAKUMBUKA KUZALIWA KWANGU AMBAPO KWA MAPENZI YA MUNGU ALIPENDA NIJE KATIKA ULIMWENGU HUU AMBA KWA SASA UMETAWALIWA NA KILA AINA YA JANGA.

NAMSHUKURU SANA MWEZI MUNGU KWA KUNILETA DUNIANI SIKU HII YA LEO, LAKINI PIA NAMSHUKURU SANA MAMA YANGU MZAZI BI ZABIBU K SELEMA KWA MIEZI TISA ALIYONIBEBA TUMBONI MWAKE NA KUNILEA MKAPA NAFIKIA HII LEO.SHUKRANI ZANGU ZA DHATI NI KWA WATU HAO WAWILI.

SHUKRANI ZANGU KWA NYOTE WENYE MAPENZI NA MIMI KWANI MLIPENDA UWEPO WANGU HAPA DUNIANI.

MUNGU ENDELEA KUNIPA UHAI, ENDELEA KUNIPA WEPESI KATIKA MAFAKIO YA MAISHA YANGU KWANI HAKUNA MWENGINE NIPASAE KUMUOMBA NA KUMUABUDU ZAIDI YAKO. AMEEN