ZANZIBAR
SHIRIKA LA BANDARI NA IDARA YA MAZINGIRA ZANZIBAR, IMETAKIWA KUWASILISHA TAARIFA YA KITAALAMU, KWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, JUU YA ATHARI ZA KIMAZINGIRA NA ZA KIMAAFA ZINAZOWEZA KUPATIKANA, KUTOKANA NA UJENZI WA HOTELI YA KITALII KARIBU NA BANDARI YA WESHA, KATIKA KIPINDI KISICHOZIDI WIKI SITA.
MAALIM SEIF AMETOA AGIZO HILO LEO WAKATI AKIFANYA MAJADILIANO MAFUPI NA VIONGOZI WA TAASISI HIZO PAMOJA NA MENEJIMENT YA HOTELI YA KITALII YA PEMBA MISALI COTTAGE, KATIKA OFISI ZA BANDARI HUKO WESHA.
AMESEMA UJENZI WA HOTELI YA KITALII YA ‘PEMBA MISALI COTTAGE’ ILIOAMBATANA NA ‘JET’ NA KUEZEKWA KWA MAKUTI WASTANI WA MITA 20 TU KUTOKA YALIPO MATANGI YA MAFUTA YA GAPCO YENYE UWEZO WA KUHIFADHI TANI 1000, NI HATARI KWA MAISHA YA BINAADAMU WAISHIO HOTELINI HAPO NA WALE WALIOKO MAENEO YOTE JIRANI.
AIDHA AMESEMA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, ITAENDELEA KUENDESHA SHUGHULI ZAKE KWA KUZINGATIA KANUNI NA SHERIA ZILIZOPO BILA YA KUMPENDELEA AU KUMUONEA MTU.
AMEZITAKA TAASISI HIZO KUKAA PAMOJA NA KUFANYA UKAGUZI WA KINA NA HATIMAE KUTAYARISHA TAARIFA ZA KITAALAMU BAADA YA IDARA YA MAZINGIRA KUANDAA HADIDU REJEA.
KATIKA KIKAO HICHO, IMEAFIKIWA MMILIKI WA HOTELI YA PEMBA MISALI COTTAGE KUGHARAMIA GHARAMA ZA UTAFITI WA KITAALAMU UTAKAOFANYIKA.
AIDHA MAALIM SEIF ALIPATA FURSA YA KUTEMBELEA BANDARI ZA WETE NA WESHA PAMOJA NA KUANGALIA MNARA WA KUONGOZEA MELI WA RAS KIGOMASHA, SAMBAMBA NA KUIKAGUA NYUMBA YA WAGENI YA’BOMAN GUEST HOUSE’ INAYOMILIKIWA NA SHIRIKA HILO.
SINGIDA
TAASISI YA KUZIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU) MKOA WA SINGIDA IMEPOKEA JUMLA TAARIFA 476 ZA TUHUMA ZA MATUKIO YA VITENDO VYA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA KATIKA KIPINDI CHA KUANZIA MWAKA 2005 HADI MWAKA HUU.
MKUU WA TAKUKURU MKOANI SINGIDA,BI JULLIANE KALLASSA AMEYASEMA HAYO LEO KATIKA SEMINA YA SIKU MOJA KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI WANAOFUNDISHA SOMO LA URAIA KATIKA SHULE ZA MKOA HUO WAKATI AKITOA HALI HALISI YA MATUKIO YALIYOPOKELEWA NA TAASISI HIYO KATIKA KIPINDI HICHO.
KWA MUJIBU WA BI. KALLASSA, KATI YA TAARIFA HIZO ZINAZOHUSU VITENDO VYA RUSHWA NI 367 WAKATI TAARIFA ZINAZOHUSU MASUALA YA UCHAGUZI NI 11 NA TAARIFA 16 KESI ZAKE ZIPO MAHAKAMANI HUKU KUKIWA NA MAJALADA MAWILI YANAHUSU TUHUMA ZA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA ULIOPITA.
AIDHA MKUU HUYO WA TAASISI YA KUZIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA HAKUWA TAYARI KUWEKA BAYANA MAJINA YA WATUHUMIWA PAMOJA NA TUHUMA ZILIZOPELEKWA KWA MWANDESDHA MASHTAKA MKUU WA SERIKALI.
HATA HIVYO HABARI AMBAZO BADO HAZIJATHIBITISHWA NA MSEMAJI HUYO ZINASEMA KWAMBA MAJALADA MAWILI YALIYOPO KWA DPP YANAWAHUSISHA WALIOKUWA WABUNGE WA MAJIMBO YA IRAMBA MASHARIKI NA IRAMBA MAGHARIBI (CCM) WALIOKUWA WAKIKABILIWA NA TUHUMA ZA KUPOKEA POSHO ZA VIKAO LICHA YA KUTOHUDHURIA KWENYE VIKAO HUSIKA VYA HALMASHAURI HIYO.
KWA MUJIBU WA HABARI HIZO TUHUMA AMBAZO BADO ZINAFANYIWA UCHUNGUZI NA TAASISI HIYO ZIMEWATAJA WALIOKUWA WAGOMBEA UBUNGE KATIKA MAJIMBO MAWILI YALIYOPO MKOANI SINGIDA YALIYOGOMBEWA NA WATU MAARUFU NA WENYE UWEZO WA KIFEDHA AMBAO HAWAKUTAJWA MAJINA.
SEMINA HIYO YA SIKU MOJA ILIANDALIWA NA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA ILIJUMUISHA WASHIRIKISHA 25 AMBAO NI WALIMU WANAOFUNDISHA SOMO LA URAIA KUTOKA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA MKOA WA SINGIDA,KATIKA WILAYA ZA IRAMBA,MANYONI,SINGIDA VIJIJINI NA MANISPAA YA SINGIDA.
DAR ES SALAAM
SHEIKH MKUU WA TANZANIA MUFTI SHAABAN BIN SIMBA, AMEITAKA JAMII NCHINI KUTAMBUA NA KUTHAMINI MICHANGO YA WALEZI NA WANAHARAKATI WANAOJITOLEA KULEA WATOTO YATIMA NA WALE WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
AMEYASEMA HAYO WAKATI WA MAHAFALI YA CHUO CHA SALAFINA ISLAMIC CENTRE KILICHOPO BUNJU NJE KIDOGO YA JIJI LA DAR ES SALAAM, AMBAPO AMESEMA UMEFIKA WAKATI KWA WAISLAMU KUTHAMINI HARAKATI HIZO KWA KUWAUNGA MKONO KWA VITENDO WALEZI HAO.
AMESEMA NI VEMA MATAJIRI WA KIISLAMU NA MSIOKUWA WAISLAMU KUJITOKEZA KUUNGA MKONO JITIHADA HIZO LI KUWAJENGEA UWEZO WA WAKUTIMIZA MALENGO NA MAAGIZO YA ALLAH (SW) NA MTUME WAKE.
AIDHA MUFTI SIMBA PAMOJA NA MWENYEKITI WA SIC, SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIR, WAMETOA SHUKRANI ZA PEKEE KWA MFADHILI WA CHUO HICHO, ABDUL ZAKARIA KWA KUWEZESHA UJENZI WA MAJENGO YA KISASA KWA MASLAHI YA DINI NA JAMII YA WATANZANIA KWA UJUMLA.
KUTOKANA NA HATUA HIYO MUFTI, AMETOA WITO NA KUWAOMBA MATAJIRI WA KIISLAMU NDANI NA NJE YA NCHI KUCHANGIA KUKIENDELEZA KIPATE MAJENGO ZAIDI KWA AJILI YA VITIVO MBALIMBALI VITAKAVYOTUMIKA KUWAJENGA VIJANA KIDUNIA NA KIAKHERA.
KWA UPANDE WAKE MWENYEKITI MTENDAJI WA TAASISI HIYO SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIR AMESEMA KUWA MAADHIMISHO YA MAHAFALI HAYO YA 12 YALIANZA TOKA MWAKA 1999 AMBAPO HADI SASA ZAIDI YA WANAFUNZI 600 WAMEHITIMU ELIMU YAO AMBAPO HIVI SASA WANAFANYAKAZI KATIKA TAASISI MBALIMBALI NCHINI.
No comments:
Post a Comment