WILAYA YA MJINI
CHAMA CHA WAKULIMA KISIWANI ZANZIBAR,(AFP) KINATARAJIA KUFANYA MATEMBEZI YA HISANI ILI KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUNUNULIA MAFUTA YA KUENDESHEA MAJENERETA 32 YACHAMA HICHO, AMBAYO HUTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA UZALISHAJI.
TAARIFA HAYO IMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MIPANGO SERA NA UENDESHAJI WA CHAMA HICHO, RASHID YUSUPH MCHENGA WAKATI AKIFANYA MAHOJIANO KATIKA KIPINDI CHA SANSETI IN ZANZABAR AMBACHO HURUSHWA NA KITUO HIKI CHA RADIO CHUCHU FM.
YUSUPH MCHENGA, AMEBAINISHA KUWA TATIZO KUBWA LINALOWAKABILIWA WAKULIMA HAPA NCHINI, NI UKOSEFU WA MIKOPO PAMOJA NA PEMBEJEO, AMBAPO AMEIOMBA SERIKALI KUTATUA MATATIZO HAYO ILI KUWAJENGEA UWEZO WAKUZALISHA KARAFUU ILIYO BORA NA KUONGEZA WIGO WA SOKO LA KIMATAIFA.
AIDHA AMEITAKA SERIKALI KUTOWAJENGEA WAKULIMA DHANA YAKUSUBIRI MPAKA WAUZE MAZAO YAO NDIPO WAPATE FEDHA ZA UZALISHAJI.
PIA MKURUGENZI HUYO AMEISHAURI SERIKALI KUSHUSHA USHURU KATIKA VYAKULA VINAVYO INGIA NCHINI ILI KUPUNGA UKALI WA MAISHA KWA WANANCHI.
ZANZIBAR
MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMEWATAKA WANANCHI WA SHEHIYA YA SANANI MUWAMBE KUACHA SHUGHULI ZA UPASUAJI MIAMBA KWA AJILI YA MATOFALI, VINGINEVYO WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
MALIM SEIF AMETOA TAHADHARI HIYO HUKO MUWAMBE ALIKOFIKA KUONA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA SERIKALI, YANAYOWATAKA WANANCHI HAO KUACHANA NA KAZI HIZO ZENYE KULETA UHARIBIFU MKUBWA WA MAZINGIRA, HUKU SERIKALI IKITAFUTA SHUGHULI MBADALA ILI WAWEZE KUJIKIMU NA MAISHA.
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, ILIPIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA UPASUAJI MIAMBA KWA AJILI YA MATOFALI, NA KUITAKA WIZARA YA KAZI, AJIRA NA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI KUTAFUTA SHUGHULI MBADALA KWA WANANCHI HAO, AMBAPO VIKUNDI 18 TAYARI VIMESHASAJILIWA KWA AJILI YA KUPATIWA MIRADI.
AIDHA AMESEMA SERIKALI HAINA NIA YA KUMUONEA MTU YEYOTE, LAKINI IKO MACHO KULINDA SHERIA ZA NCHI NA KUHIFADHI MAZINGIRA YAKE, HIVYO MTU YEYOTE ATAKAEPATIKANA KUHUSIKA NA VITENDO HIVYO ATACHUKULIWA HATUA KALI.
AMEMTAKA MKUU WA WILAYA YA MKOANI KUSHIRIKIANA NA SHEHA WA SHEHIYA HIYO PAMOJA NA WANANCHI KUONA TATIZO HILO LINAONDOKA KABISA KWA MASLAHI YA TAIFA NA KIZAZI CHAO.
KITENDO VYA UPASUAJI WA MIAMBA HIYO KIMETAJWA KKUWA NA ATHARI KUBWA KWA WANANCHI WENYEWE KWA KUZINGATIA MASHIMO HAYO MAKUBWA YAMEZUNGUKA NYUMBA ZAO NA KUHATARISHA MAISHA YA WATOTO WADOGO AU WAGENI WANAOTEMBELEO ENEO HILO.
AIDHA MAALIM SEIF AMESEMA SERIKALI IKO KATIKA HARAKATI ZA KUWATAFUTIA WANANCHI WA KIJIJI HICHO NJIA MBADALA, HIVYO AMELIAGIZA PIA JESHI LA POILISI MKOA WA KASKAZINI PEMBA KUSAIDIA ULINZI KATIKA MAENEO HAYO.
ZANZIBAR
BAADA YA SAKATA LA MIKATABA YENYE UTATA KATIKA BARAZA LA MANISPAA, MEYA WA ZANZIBAR, KHATIB ABRAHMAN KHATIB, AMESEMA HIVI SASA WANAJIANDAA KUONA WATENDAJI WA BARAZA HILO WANATEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZAKE.
AMEYASEMA HAYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, HUKO AFISINI KWAKE MALINDI MJINI ZANZIBAR WALIOFUATILIA UTEKELEZAJI WA RIPOTI YA BARAZA HILO BAADA YA KUANDAA MAPENDEKEZO JUU YA SAKATA LA MIKATABA YENYE UTATA AMBAYO SASA YAPO SERIKALINI KUSUBIRI UAMUZI WAKE.
HIVI KARIBUNI WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WALIISHUPALIA BAJETI YA AFISI YA RAIS IKULU, KWA KULISAKAMA BARAZA HILO JUU YA UTENDAJI KAZI ZAKE NA TUHUMA KUWAPO KWA HARUFU YA RUSHWA ILIYOTEMBEZWA KWA BAADHI YA WATENDAJI AMBAPO WAJUMBE HAO WALITAKA KUJUA MAPENDEKEZO YALIOMO KATIKA RIPOTI HIYO.
MEYA WA MANISPAA HIYO AMESEMA ILI KUWEZA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA TAASISI HIYO HIVI SASA WANACHOKUSUDIA KUKIFANYA NI LAZIMA WATENDAJI WAKUBALI KUONA WANAFUATA SHERIA NA KANUNI ZA BARAZA HILO AMBAPO KILA MFANYAKAZI ATAPASWA KUZIFUATA.
AIDHA AMESEMA TATIZO MBALO LILIBAINIKA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BARAZA HILO KULIKOSEKANA TARATIBU ZA KUFUATA SHERIA KATIKA BAADHI YA MAMBO NA MAAMUZI YALIOKUWA YAKIFANYIKA KIHOLELA.
AMESEMA HIVI SASA TAYARI BARAZA HILO LIMESHAPITISHA BAJETI YAKE AMBAYO INAKUSUDIA KUTUMIA, AMBAYO NI ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 3.7 KWA SHUGHULI ZA BARAZA HILO KWA MWAKA UJAO WA FEDHA WA 2011/2012.
MOROGORO
MAJERUHI WATATU KATI YA 20 WA AJALI YA BASI LA HOOD, ILIYOTOKEA JUZI KATIKA HIFADHI YA WANYAMAPORI MIKUMI, MKOANI MOROGORO WALIOLAZWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA HUO, WANATARAJIWA KUPELEKWA KATIKA TAASISI YA MIFUPA "MOI", PAMOJA NA HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM ILI WAWEZE KUPATIWA MATIBABU ZAIDI BAADA YA HALI ZAO KUONEKANA
KUWA MBAYA.
HAYO YAMEBAINISHWA NA MGANGA MKUU WA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO FRIDA MOKITI, WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI HOSPITALINI HAPO, KUHUSU HALI ZA MAJERUHI HAO.
MGANGA MKUU HUYO AMESEMA KATI YA MAJERUHI HAO MMOJA NI MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA (11), ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JEMIMA ZAMBI HUKU AKISHINDWA KUWATAJA WENGINE, NA KUDAI KUWA BADO MADAKTARI WANAPITA KUKAGUA WAGONGWA NA KWAMBA HUENDA IDADI YAO IKAONGEZEKA.
AIDHA AMESEMA KATI YA HAO WATATU WALIRUHUSIWA, NA KWAMBA HOSPITALI HIYO ILIPOKEA MAJERUHI 41 AMBAPO WENGINE WALIRUHUSIWA NA KUBAKI 21 HUKU WATATU WAMERUHUSIWA LEO.
HATA HIVYO AMESEMA HALI YA MADAWA KATIKA HOSPITALI HIYO SIYO MBAYA, NA KWAMBA WALIPATA MSAADA WA BAADHI YA MADAWA YALIYOPUNGUA KUTOKA KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JITU PATEL.
KWA UPANDE WAKE MMILIKI WA KAMPUNI YA MABASI YA HOOD, MOHAMED HOOD AMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA AJALI HIYO NA KUAHIDI KUTOA MSAADA KWA NDUGU WA MAREHEMU WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI HIYO PAMOJA NA KUWASAIDIA MAJERUHI.
No comments:
Post a Comment