Jul 17, 2011

ZANZIBAR

VIJANA NCHINI WAMETAKIWA KUWA TAYARI KUFANYA KAZI ZA KUJITOLEA ZENYE MANUFAA KWAO NA TAIFA.

HAYO YAMEELEZWA LEO NA MAKAMU WA PILI WA RAIS, BALOZI SEIF ALI IDDI,WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI ENDELEVU YA USAFI WA MAZINGIRA ILIYOANDALIWA NA JUMUIYA ISIYO YA KISERIKALI YA ZASOSE KATIKA UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZAMANI MNAZI MMOJA.

BALOZI SEIF AMESEMA VIJANA WANAPASWA KUFAHAMU KWAMBA WAZANZIBARI NA WATANZANIA LAZIMA WAFANYEKAZI WENYEWE NA KUACHA TABIA YA UTEGEMEZI.

BALOZI SEIF AMETOA HISTORIA YA KUFANYA KAZI ZA KUJITOLEA ILIFANYIKA MIAKA MINGI NA KUWEZA KUJIPATIA UMAARUFU NI PAMOJA NA UJENZI WA NYUMBA ZA MAENDELEO,UNGUJA NA PEMBA,UJENZI WA UWANJA WA AMAAN,UJENZI WA BARABARA MBALI MBALI,SKULI NA MAMBO MBALI AMBAYO YAMEWEZA KULETA MAENDELEO MAKUBWA YA NCHI.

AMEWATAKA VIJANA KUFAHAMU KUA HAKUNA SHUGHULI ZA MAENDELEO ZILIZOFANYIKA KISIWANI ZANZIBAR BILA YA NGUVU ZA VIJANA AMBAPO KWA PAMOJA WALIAMUA KUJITOLEA.

AIDHA BALOZI SEIF AMEPONGEZA VIJANA NA HASA JUMUIYA YA ZASOSE KWA KUFANYA UAMUZI WA KUANZISHA KAMPENI YA USAFI UNAOTOKANA NA KUGUSWA NA TAMKO LA RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMMED SHEIN LILILOSEMA KUWA HALI YA MJI WA ZANZIBAR HAIRIDHISHI.

KWA UPANDE WAKE KATIBU MTENDAJI WA JUMUIYA HIYO, SHAKA HAMDU SHAKA AMESEMA KUWA LENGO KUU LA KUANZISHA JUMUIYA HIYO NI KUSIMAMIA,KUHAKIKISHA NA KUTOA MUAMKO KWA VIJANA NA JAMII JUU YA SUALA LA USAFI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA.

KATIKA UZINDUZI HUO, JUMLA YA SHILINGI MILIONI 2,600,000 ZIMEKUSANYWA KWA AJILI YA KUCHANGIA JUMIYA HIYO HUKU AMBAPO WENGINE WAMEAHIDI KUTOA JUMLA YA SHILINGI MILIONI 5,555,000 TANO LAKI TANO NA HAMSINI ELF.

ZANZIBAR

WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NA USHIRIKA IMESEMA ITAENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WA ELIMU WANAUSHIRIKA NA WAJASIRIAMALI WENGINE KAMA MBINU YA KUWAPA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WA KUZALISHA BIDHAA BORA NA KUKUZA FURSA ZA AJIRA.

AKITOA MAELEKEZO KWA WAJASRIAMALI WALIOKUWA WAKIJIANDAA KWENDA MWANZA KWA MAFUNZO YA UJASIAMALI, KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO, ASHA ALI ABDULLA AMESEMA SERIKALI ITAFIKIA LENGO HILO KWA WATU WENGI ZAIDI.

AIDHA AMESEMA KATIKA KIPINDI AMBACHO NI CHA USHINDANI WA KIBISHARA NA HUDUMA WAJASIRIAMALI ZANZIBAR LAZIMA WABADILIKE NA KUTEGENEZA BIDHAA ZITAKAZOMUDU USHINDANI KATIKAMASOKO YA KIBIASHARA NCHINI

WAJASIRIAMALI WANAOHUDHURIA MAFUNZO YA MATUMIZI YA NGOZI KUTENGENEZA VIATU AINA YA KUBADHI KUTOKA PEMBA NA UNGUJA WAMETAKIWA KUWA MAKINI KATIKA MAFUNZO HAYO NA KUCHUKUA ELIMU ILI WATAKAPORUDI NYUMBANI WAWE WALIMU KWA WENZAO.

ZIARA HIYO IMEGHARAMIWA NA SERIKALI KUPITIA WIZARA KAZI NA UWEZESHAJI KWA KUSHIRIKIANA NA WAWAKILISHI WA MAJIMBO YA KIKWAJUNI NA WAWI PEMBA.

KWA UPANDE WAKE KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO, ALI JUMA AMESEMA INASHANGAZA KUONA BIDHAA NYINGI ZINAZOTOKANA NA SANAA ZA MIKONO KATIKA MJI WA ZANZIBAR HAZITOKI ZANZIBAR.

AMESEMA BIDHAA NYINGI NA SANAA ZINATOKA NJE YA ZANZIBAR HIVYO HAZIONESHI UTAMADUNI HALISI WA ZANZIBAR AMBAPO AMEWATA WAJASIRIAMALI KUWA WABUNIFU ZAIDI ILI KULETA USHINDANI KIBIASHARA.

WILAYA YA MJINI MAGHARIBI

KATIBU MTENDAJI JUMUIYA YA KUHIFADHI MAZINGIRA RAS FUMBA (FUPECO), ABDULRAZAK SHAABAN JUMA, AMESEMA LENGO LA KUANZISHWA JUMUIYA HIYO NI KUHIFADHI MAZINGIRA YA BAHARINI NA NCHI KAVU ILI KULETA MAENDELEO ENDELEVU NA USTAWI WA WANAJAMII WA FUMBA.

AMEYASEMA HAYO HII LEO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUMALIZIKA KAMPENI YA USAFI KATIKA MAENEO YA FUKWE YA BAHARI YA KORORO ILIYOPO FUMBA, WILAYA YA MAGHARIBI.

JUMUIYA HIYO IMEAMUA KUFANYA USAFI KATIKA MAENEO YA FUKWE HIYO KUTOKANA NA MAZINGIRA YAKE KUWA KATIKA HALI MBAYA INAYOWEZA KULETEA ATHARI KWA VIUMBE WA BAHARINI NA NCHI KAVU.

JUMA AMEELEZA KUWA JUMUIYA HIYO IMEANZA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ILI KUREJESHA MANDHARI YA ASILI KATIKA FUKWE HIYO ILI KUWEZE KUPATIKANA KWA MAENDELEO YA ZANZIBAR.

AIDHA AMESEMA MAZINGIRA YA BAHARI HIYO YAMEATHIRIWA VIBAYA NA UTUPAJI TAKA, MIFUKO YA PLASTIKI, UCHIMBAJI MCHANGA NA UKATAJI MITI OVYO KWA AJILI YA KUTENGENEZA MAKAA.

AKIZUNGUMZIA CHANGAMOTO ZA JUMUIYA HIYO, AMESEMA NI PAMOJA NA UKOSEFU WA VITENDEA KAZI KAMA MAPANGA VIATU MAALUM, MABARO GLAVU KUZUIA UCHAFU NA VIFAA VYENGINE VIDOGO VIDOGO.

HIVYO, AMEWATAKA WAFADHILI MBALI MBALI KUJITOKEZA KATIKA KUIUNGA MKONO JUMUIYA HIYO AMBAYO BADO NI CHANGA ILI IWEZE KUFANYA KAZI ZAKE KWA UFANISI ZAIDI.

No comments:

Post a Comment