Oct 2, 2009

VIZURI VITATUUA JAMANI

Na Mfaume Pastory




VIZURI VITATUUA JAMANI!



Habari za wakati mpenzi msomaji matumaini yangu ni mzima wa afya njema kabisa hapo ulipo, sote hatunabudi kumshukuru muumba kwa kutukutanisha tene siku nyingine nzuri hii ya leo.

Liati kama tungelikuwa na uwezo wa kubashiri au kuyaona yatakayotutokea mbeleni basi hakika yale ya shari! yasingelitupata.

Nakumbuka ilikuwa ni ijumaa nzuri ya February 25 2005 siku ambayo asubuhi na mapema niliamka na sehemu yangu ya kwanza kwenda baada ya kutoka nyumbani ilikuwa ni shirika la reli Tabora.

Kwa kawaida na mazoea niliyokuwa nayo kipindi hicho ilikuwa mara baada kumaliza mizunguko yangu yote jioni saa 12 nililazimika nipite kumjulia hali rafiki yangu kipenzi wakike aliyejulikana kwa jina la Eva Mwamba.

Ama kwa hakika katika wasichana waliobahatika kubarikiwa uzuri, wenye kujipamba na wakapambika na wakipita kutazamwa mara mbilimbili! Eva ni mingoni mwao.

Alikuwa si mrefu wala si mfupi ila ni wakawaida, mwenye umbo zuri mnene wakawaida, mwenye midomo na macho yakuvutia. Wahenga walisema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza, msomaji hali hii ilimfanya Eva kupendwa na vijana wengi ingawa wakati huo mimi ndiye nilikuiwa chaguo lake.

Sefu alikuwa ni miongoni mwavijana waliopata bahati ya kukutana na Eva na alivutiwa nae wakati huo Sefu alikuwa akilitumikia jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ) na bila kuchelewa alipanga mikakati ya jinsi gani angeliweza kuwa mahusiano ya kimapenzi na Eva wakati huo akiwa kidato cha pili umri miaka 17.

Katika harakati zake Sefu aliweza kupata taarifa nyingi sana zilizo husu mahusiano yetu baina yangu na Eva na alitamani siku aje kifahamu mimi ni mtu wa aina gani.

Enzi hizo nikiwa kiwa kidato cha nne katika shule moja Mkoani Tabora iliyojulikana kwa jina la Uyui High school. Alibahatika kuniona na baada ya kuniona aliahidi kuvunja mahusiano yetu kwanamna yeyote ile kwakuwa yeye ni mwanajeshi wa jeshi la wananchi Tanzania!

Mpenzi msomaji, Sefu alitumia pesa nyingi! Alitumia zawadi za ina mbalimbali! lakini jitihada zake zote ziligonga mwamba na ndipo alipoamua kutumia nafasi yake ya uanajeshi aliyopewa na serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Mungu si athumani February 25,2005 saa 12 jioni nikiwa na rafiki yangu kwa jina Sospeter Maganga, tulipita nyumbani anakoishi Eva ili kumjulia hali ndipo tulipokutana na askari Sefu naye akiwa katika mawindo yake.

Wakati wote baada ya yeye kuwa amefika nyumbani kwao Eva hakufanikiwa kumtoa wala kuonana ila mimi nilipofika tu nilituma ujumbe na muda mfupi tu Eva alifika na tukaelekea sehemu ambayo tulipenda kufanyia mazungumzo yetu.

La hasha! Hatukuwa na hili wala lile tulimwona Sefu akija kwa kasi , mlengwa nikiwa ni mimi na alifika pale tulipokuwa tumekaa pasi kuuliza alipiga bara bara amahakika nahisi alijaribu kukumbushia mazoezi yale ambayo alifundishwa enzi za mafunzo yake ya akiwa mafunzoni.

Eva na Sospeter hawakuwa na jinsi walibidi kukaa mbali kukiepuka kichapo, katika harakati za kujaribu kujiokoa nilifanikiwa kukimbia na nilipofika umbali mfupi tu nilianguka na kuzimia palepale! Wizara ya Elimu karibu na kumbi maarufu ya jashi muungano mesi.

Inasikitisha sana! Kwasasa Eva hajaolewa ila tayari anafamilia! hii nikutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake. Hakika hiyo ni siku ambayo sintokaa ni isahau katika maisha yangu yote.


Tatizo kubwa ni ujinga ambao watanzania wachache bado wanao miongoni mwao, kutumia dhamana walizokabidhiwa na serikali kinyume na sheria kwa kukiuka haki za raia wataifa lake! Kukiuka maadili ya jamii kwa kuwatamani kimapenzi watoto! ambao ni sawa na watoto wao hatimae kuwapotezea malengo na mwelekeo wa maisha yao.

Nashukuru kwa hivi sasa kuona baadhi ya taasisi na vyombo nchini vikipambana katika kupigania haki za watoto wakike, mfano Haki Elimu wakiwa na dhamira ya kumjengea msingi bora ya wamaisha mototo wa kike kwani walio wengi wamejikuta hawana mwelekeo kwa kupata mimba zisizo tarajiwa kwa kudanganywa.

Ndugu zangu si viongozi pekee wa serikali wanaopaswa kukemea wale wanaojaribu kukiuka sheria na maadili nchini bali hata wewe raia pia unalojukumu hilo kwa kuwafikisha katika vyombo vya sheria watu kama hao.

Tusisite kuwashitaki wale wote tunaowaona wakivunja sheria na kutenda maovu katika ajamii zetu kwani mahakama na vyombo vingine vya sheria vipo kwa ajili yetu raia basi nasi nijukumu letu kuvitumia.