Diwani wa kata ya misufini Salum Mfamaji ambaye pia ni mjumbe wa baraza la
katiba manispaa ya songea amewataka wajumbe ambao wanajadili rasimu ya katiba
kwa manispaa ya songea kujadili mawazo
ambayo yametolewa na wananchi na sio kwa manufaa ya vyama vyao.
Amesema ni lazima wajumbe ambao wamechaguliwa na wananchi kuwawakilisha
wananchi wao kikamilifu badala ya kuangalia maslahi yao binafsi.
Wajumbe wa mabaraza ya mabadiliko ya katiba manispaa ya songea leo wameanza
kujadili rasimu iliyopendekezwa na wananchi kwenye mchakato wa kupata maoni ya
katiba mjadala ambao utakuwa wa siku tatu kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu
matogoro.
Wizara ya
Afya na Ustawi wa jamii imeombwa kuanzisha kliniki katika hospitali na vituo
vya Afya nchini kwa ajiLi ya walemavu wa ngozi Albino walio athirika na ugonjwa
wa saratani ya ngozi ili waathirika hao waweze kutambulika na kupatiwa tiba
badala ya kuwapatia dawa za kuzuia mionzi ya jua.
Mwenyekiti
wa chama cha Albino nchini Ernest Kimaya ameitaka idara ya ustawi wa jamii
kuandaa bajeti itakayosaidia Maalbino nchini kupata huduma ya afya stahiki.
Aidha
kimaya amesema kuwa hadi hivi sasa tayari wamesha fanya mazungumzo na wizara na
wameanza kutoa dawa ya kuzuia mionzi ya jua katika sehemu mbali mbali nchini.
Wachimbaji
wadogo wa madini katika mgodi wa Mererani jijini Arusha wameitaka serikali kusikiliza madai yao kama
wanavyowasikiliza wawekezaji kutoka nje.
Mmoja wa
wachimbaji hao wadogo Jackson Manjuu amesema pindi wanapokuwa na mgogoro baina
yao na wawekezaji huonekana kuegemewa au kupendelewa zaidi kwa wawekezaji bila
kuwajali wachimbaji wadogo ambao ni wazawa.
Manjuu
amesema kuwa ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima serikali haina budi kutenga
maeneo maalumu kwa ajili ya wazawa.
No comments:
Post a Comment