Aug 3, 2013

HABARI KUTOKA RUVUMA

KUTOKA SONGEA RUVUMA TANZANIA

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki amewata wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pindi wanapowaona watu wahalifu ambao wanaenda kinyume na sheria katika jamii inayowazunguka.

Amesema jeshi la polisi limejipanga kudhibiti vitendo vya uhalifu ambavyo vinaendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali yaliyopo ndani ya mkoa.

INSERT..............KAMANDA SAUTI.

Ameyasema hayo baada ya jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa wa makambi uliopo manispaa ya songea kumshikilia mwaharifu ambaye amekutwa na risasi kumi za silaa aina ya SMG anayejulikana kwa jina Mhamed mhamed mwenye umri wa miaka arobaini.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Katibu wa umoja wa wanawake wilaya ya Songea vijijini UWT Selina Ngonyani amewataka wanaume kutoa ushirikiano kwa familia zao kwa kutoa huduma zote za msingi ambazo zinahitajika katika familia zao.

amesema wazazi wote washirikiane kwa pamoja  kwa kupangilia kipato ambacho wanakipata katika msimu huu wa mavuno ili waweze kuberesha maendeleo ya pamoja katika familia zao wanazoishi.

INSERT........UWT SAUTI.

Kwa upande wa mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM songea vijijini Nely Duwe amesema wazazi wote hawana budi kushirikiana ili kuweza kupata maendeleo kwa kusomesha watoto wao na kuberesha maisha yao.

INSERT..............MWENYEKITI SAUTI.

Kwa upande mwingine wamewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo wamepewa wananchi waliojiunga katika vikundi mbalimbali katika jimbo la peramiho waliyopewa na Mbunge wa jimbo la Peramiho Jenestha Mhagama ukiwemo mradi wa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.

1 comment: