Jul 19, 2011

ZANZIBAR

WIZARA YA MIUNDO MBINU NA MAWASILIANO IMESEMA HAITOWEZA KUZITEKELEZA AHADI ZILIZOTOLEWA NA MARAIS WALIOONDOKA MADARAKANI ZA KUZIFANYIA MATENGENEZO BARABARA ZA NDANI KWA WAKATI MMOJA NA BADALA YAKE ITAFANYA KAZI HIYO HATUA KWA HATUA.

NAIBU WAZIRI WA WIZARA HIYO, ISSA HAJI USSI AMETOA UFAFANUZI HUO BARAZANI HII LEO WAKATI AKIJIBU SUALI LA MWAKILISHI WA KWAMTIPURA HAMZA HASSAN JUMA.

MWAKILISAHI HUYO ALITAKA KUJUA LINI SERIKALI ITATEKELEZA AHADI ZA MARAIS WALIOPITA KATIKA KUZIFANYIA MATENGEZO BARABARA ZA NDANI IKIWEMO YA MBORIBORINI.

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MIUNDOMBINU AMEKIRI KUWEPO AHADI HIZO NA KUSEMA ZINATHAMINIWA NA KUHESHIMIWA NA WIZARA YAKE INAZIHESHIMU, LAKINI ZINASHINDWA KUTIMIZWA KWA WAKATI MMOJA.

AMESEMA WIZARA HIYO ITAHAKIKISHA KUWA INALIONDOA TATIZO HILO KILA PALE ITAPOKUWA INAPATA UWEZO KWANI HIVI SASA WAMEANZA KUPUNGUZA MOJA BAADA NYENGINE.

AIDHA AMEWATAKA WANANCHI WASIVUNJIKE MOYO KUTOKANA NA WIZARA HIYO KUZIFANYIAKAZI AHADI ZOTE ZA UJENZI WA BARABARA INAYOANZIA KWA ABASI HUSSEIN KUPITIA MBORIBORINI HADI AMANI DARAJA BOVU.

ZANZIBAR

BAADHI YA WAWAKILISHI WA BARAZA LA SERIKALKI YA MAPINDUZI ZANZIBAR, WAMETOA WITO KWA WIZARA YA KAZI UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NA USHIRIKA, KUANDAA MPANGO UTAKAOTOA ELIMU KWA VIJANA ITAKAYO WAWEZESHA KUJIARI, NA KUWAPATIA MIKOPO ITAKAYO WASAIDIA KUANZISHA MIRADI YAO.

WITO HUO UMETOLEWA LEO NA WAWAKILISHI KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA WAWAKILISHI, WAKATI WAKICHANGIA HOJA ZAO JUU YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA KAZI UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NA USHIRIKA.

AKIZUNGUMZA KATIKA BARAZA HILO MWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI SALMIN AWARI, AMEBAINISHA KUA TATIZO KUBWA LINALOWAKABILI VIJANA NI UKOSEFU WA AJIRA AMBAPO AMESEMA LINATOKANA NA DHANA KUWA, VIJANA WENGI WANASHINDWA KUJIAJIRI.

SERIKALI KWA UPANDE WAKE INASEMA HAINA UWEZO WA KUAJIRI WATU WOTE, HIVYO NI VYEMA KWA SASA WANACHI WAELEKEZE NGUVU ZAO KATIKA KUJIAJIRI WENYEWE.

PAMOJA NA KAULI HIYO YA SERIKALI, ELIMU IMETAJWA KUWA MSINGI MUHIMU KATIKA KUWAJENGEA VIJANA UWEZO WAKUJIAJIRI HIVYO SERIKALI IMESHAURIWA PIA KUSHIRIKIANA KIKAMILIFU NA TAASISI ZINAZOHUSIKA KATIKA KUWAWEZESHA VIJANA ILI KUTATUA TATIZO HILO.

AIDHA WAWAKILISHI WAMEITAKA SERIKALI NA WIZARA HUSIKA KUWEKA WAZI SIFA ZITAKAZO MWEZESHA MWANANCHI KUPATA MKOPO ILI WANANCHI WAPATE KUZIFAHAMU.

IMEBAINISHWA KUWA ENDAPO SERIKALI ITAAMUA KUIWEZESHA SEKTA YA AJIRA, BASI TATIZO LA AJIRA NA UMASIKINI LITAONDOKA MIONGONI MWA WANANCHI WAKE.

ZANZIBAR

SERIKALI YA ZANZIBAR IMESEMA KUWA INASHINDWA KUIRUHUSU HOSPITALI INAYOMILIKIWA NA JESHI LA WANANCHI KATIKA KIJIJI CHA WAWI KISIWANI PEMBA, KUTOA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA UKIMWI ARV KUTOKANA NA KUKOSA SIFA YA WAHUDUMU MAALUM WA KUDUMU KATIKA HOSPITALI HIYO.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, SIRA UBWA MAMBOYA, AMETOAUFAFANUZI HUO KUFUATIA SUALI ALILOULIZWA BARAZANI NA MWAKILISHI WA JIMBO HILO, SALEH NASSOR.

MWAKILISHI HAYO AMETAKA KUJUA KWANINI HOSPITALI HIYO HAIRUHUSIWI KUTOA DAWA ZA ARV INGAWA IMETENGENEZWA KWA MFUMO WA KISASA.

NAIBU WAZIRI HUYO AMESEMA WIZARA YAKE INASHINDWA KUWEKA DAWA HIZO KATIKA KITUO HICHO KWA VILE HAKUNA DAKTARI AMBAYE ATAWEZA KUKAA MUDA WOTE JAMBO AMBALO LINAIFANYA WIZARA HIYO KUSHINDWA KURUHUSU UTOAJI WA DAWA HIZO KATIKA HOSPITALI HIYO.

AIDHA AMESEMA HALI HIYO WANALAZIMIKA KUSHINDWA KWA KUFANYA HIVYO KUTOKANA NA KAZI AMBAZO ZINAHITAJIKA KUFANYIKA WAKATI WA UTOAJI DAWA HIZO HULAZIMIKA KUTOLEWA USHAURI JAMBO AMBALO LITAKOSEKANA IKIWA HAKUNA DAKTARI KWA MUDA WOTE.

AMESEMA DAWA ZA ARV, ZIMEAMUALIWA KUTOLEWA KATIKA VITUO MAALUM IKIWA NI HATUA YA WIZARA HIYO KUWEKA UTARATIBU MZURI WA UTOAJI DAWA HIZO KATIKA HOSPITALI ZA SERIKALI.

AMESEMA IKIWA HOSPITALI YA WAWI ITAWEZA KUPATA DAKTARI ATAESIMAMIA UTOAJI WA DAWA HIZO, WIZARA HIYO HAITASITA KUFANYA HIVYO KWANI DHAMIRA YA SERIKALI KUHAKIKISHA KUNAKUWA NA UTARATIBU MZURI WA AFYA.

ZANZIBAR

SERIKALI INAHITAJI SHILINGI BILIONI 120 KUONDOA TATIZO LA UPATIKANAJI MAJI SAFI NA SALAMA KATIKA MKOA WA MJINI MAGHARIBI.

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAKAAZI, ARDHI, MAJI NA NISHATI HAJI MWADINI MAKAME AMEYASEMA HAYO LEO WAKATI AKIJIBU SUALI LA NYONGEZA LA MWAKILISHI WA VITI MAALUM VIWE KHAMIS ABDALLA, ALIYETAKA KUJUA LINI TATIZO LA MAJI KATIKA MAENEO HAYO LITAMALIZIKA.

NAIBU WAZIRI AMESEMA NI KWELI TATIZO LA MAJI KATIKA MAENEO YA MJINI NI KUBWA KIASI AMBACHO SERIKALI ITAHITAJI KUWA NA SHILINGI BILIONI 120 ILI KUWEZA KUKABILIANA NA TATIZO HILO NA KUMALIZIKA KABISA.

AMESEMA KUTOKANA NA HALI HIYO, WIZARA YAKE IMEAMUA KUTENGA SHILINGI MILIONI 40 NDANI YA KIPINDI CHA MIAKA MITATU KUWEZA KUONDOA TATIZO HILO KWA UNGUJA NA PEMBA.

AKITA SABABU ZILIZOPELEKEA HALI HIYO NIPAMOJA NA BAADHI YA WANANCHI KUJENGA MAHODHI MAKUBWA CHINI YA ARDHI YANAYOSABABISHA SEHEMU KUBWA YAHUDUMA HIYO KUTUMIWA NA WATU WACHACHE.

AMEBAINI TATIZO JINGINE TATIZO JENGINE NI UCHAKAVU WA MIUNDO MBINU YA USAMBAZAJI WA HUDUMA YA MAJI NA UJENZI HOLELA UNAOFANYIKA KATIKA VYANZO VYA MAJI NA MTANDAO WA MAJI HUKU MAHODHI YALIOJENGWA YAKIWA HAYAKO KITAALAMU.

WILAYA YA MJINI

WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO WAMEIOMBA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, KUWAWEZESHA KWA KUWAPATIA MIKOPO AMBAYO ITAWASAIDIA KUJIENDELEZA KIMAISHA.

HAYO YAMEELEZWA NA MFANYABIASHARA MMOJA, MUSSA NASSOR OMAR WAKATI AKIZUNGUMZA NA CHUCHU FM HAPO OFISINI KWAKE MICHEZANI MJINI UNGUJA.

AIDHA MUSSA AMESEMA IWAPO SERIKALI ITAWAWEZESHA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO KWA KUWAPATIA MIKOPO MBALINBALI, WATAWEZA KUONDOKANA NA HALI YA UTEGEMEZI, PAMOJA NA KUKAA MASKANI NA KUWEZA KUEPUKANA NA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA.

MUSSA AMESEMA ANAJISHUGHULISHA NA KAZI YA USHONAJI WA VIATU AMBAYO KAZI YAKE HIYO, IMEKUWA IKIMPATIA KIPATO KIASI AMBACHO AMEWEZA KUJIKIMU KIMAISHA PAMOJA NA KUWASOMESHA WATOTO WAKE.

SAMBAMBA NA HAYO AMEWATAKA VIJANA KUJISHUGHULISHA NA KAZI MBALIMBALI, AMBAZO ZITAWEZA KUWAPATIA AJIRA NA KUWACHA KUTEGEMEA AJIRA KUTOKA SERIKALINI.

No comments:

Post a Comment