Aug 19, 2013

HABARI TOKA RUVUMA TANZANIA


Diwani wa kata ya misufini Salum Mfamaji ambaye pia ni mjumbe wa baraza la katiba manispaa ya songea amewataka wajumbe ambao wanajadili rasimu ya katiba kwa manispaa ya songea kujadili mawazo  ambayo yametolewa na wananchi na sio kwa manufaa ya vyama vyao.

Amesema ni lazima wajumbe ambao wamechaguliwa na wananchi kuwawakilisha wananchi wao kikamilifu badala ya kuangalia maslahi yao binafsi.

Wajumbe wa mabaraza ya mabadiliko ya katiba manispaa ya songea leo wameanza kujadili rasimu iliyopendekezwa na wananchi kwenye mchakato wa kupata maoni ya katiba mjadala ambao utakuwa wa siku tatu kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu matogoro.


Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imeombwa kuanzisha kliniki katika hospitali na vituo vya Afya nchini kwa ajiLi ya walemavu wa ngozi Albino walio athirika na ugonjwa wa saratani ya ngozi ili waathirika hao waweze kutambulika na kupatiwa tiba badala ya kuwapatia dawa za kuzuia mionzi ya jua.

Mwenyekiti wa chama cha Albino nchini Ernest Kimaya ameitaka idara ya ustawi wa jamii kuandaa  bajeti  itakayosaidia Maalbino nchini  kupata huduma ya afya stahiki.

Aidha kimaya amesema kuwa hadi hivi sasa tayari wamesha fanya mazungumzo na wizara na wameanza kutoa dawa ya kuzuia mionzi ya jua katika sehemu mbali mbali nchini.



Wachimbaji wadogo wa madini katika mgodi wa Mererani jijini Arusha  wameitaka serikali kusikiliza madai yao kama wanavyowasikiliza wawekezaji kutoka nje.

Mmoja wa wachimbaji hao wadogo Jackson Manjuu amesema pindi wanapokuwa na mgogoro baina yao na wawekezaji huonekana kuegemewa au kupendelewa zaidi kwa wawekezaji bila kuwajali wachimbaji wadogo ambao ni wazawa.

Manjuu amesema kuwa ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima serikali haina budi kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wazawa.

No comments:

Post a Comment