Jul 9, 2011

JULY 9-2011

ZANZIBAR

MAWAZIRI WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO ILI KUJENGA JUMUIYA YENYE NGUVU BARANI AFRIKA.

USHAURI HUO UMETOLEWA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMAD OFISINI KWAKE MIGOMBANI, ALIPOKUWA NA MAZUNGUMZO NA MAWAZIRI HAO PAMOJA NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZILIZOMO KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

MAALIM AMESEMA HATUA HIYO NI MUHIMU ILI KUIPA NGUVU JUMUIYA HIYO IWEZE KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZILIZOPO PAMOJA NA KUWAUNGANISHA WANANCHI WAKE AMBAO WANA UHUSIANO WA KINDUGU KWA MUDA MREFU.

AMEKITAKA CHOMBO HICHO KITUMIKE IPASAVYO KAMA KIUNGO MUHIMU CHA KUZIUNGANISHA NCHI WANACHAMA KWA FAIDA YA NCHI HIZO NA WATU WAO.

AIDHA MAALIM SEIF AMEWAELEZEA VIONGOZI HAO MAFANIKIO YA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA, AMBAPO AMESEMA IMESAIDIA KUWEPO KWA HALI YA UTULIVU NA AMANI PAMOJA NA USHIRIKIANO MIONGONO MWA WATU WAKE.

PEMBA

AFISA MDHAMINI WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI PEMBA, DK, SULEIMAN SHEHE MOHAMMED, AMEKIPONGEZA KIKUNDI CHA USHIRIKA CHA JITUME SACCOS CHA MWAMBE MKOA WA KUSINI PEMBA, KWA UAMUZI WAKE WA KUANZISHA MRADI MBADALA WA KUENDELEZA USHIRIKA WAO NA KUJIEPUSHA NA MIRADI INAYOHARIBU MAZINGIRA.

AMESEMA KUWA UAMUZI WA KUACHA KUCHIMBA MAWE NA KOKOTO NA KUAMUA KUJISHUGHULISHA NA KILIMO NI WA KIJASIRI NA HATUA HIYO INAENDANA NA MALENGO YA SERIKALI YA KUWATAFUTIA MIRADI MBADALA WALE WOTE WANAOJISHUGHULISHA NA KAZI KAMA HIZO ILI KULINDA NA KUHUIFADHI MAZINGIRA.

SERIKALI YA ZANZIBAR KUPITIA WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI IMEANDAA UTARATIBU WA MIKOPO KWA VIKUNDI KAMA HIVYO VYA KILIMO ILI KUSAIDIA JUHUDI ZAO SAMBAMBA NA KUTAFUTA WAFADHILI KUSAIDIA MAPINDUZI YA KILIMO HASA CHA UMWAGILIAJI MAJI ILI WAKULIMA WAWEZE KUPATA MAPATO ZAIDI.

AIDHA AMESEMA SERIKALI IMEAMUA MAKUSUDI KUPUNGUZA BEI ZA PEMBEJEO ZA KILIMO ILI KUWAFANYA WAKULIMA WAMUDU KUZINUNUA, NA KUPUNGUZA KILIO CHA UKOSEFU NA BEI GHALI ZA PEMBEJEO .

NAE KATIBU WA KIKUNDI HICHO SILIMA HAJI NGWALI, AMESEMA BAADA YA KUANZISHA KILIMO CHA KUNDE EKARI SITA, WAMEANZA KUONA FAIDA YAKE NA WANAKUSUDIA KUONGEZA MIRADI MIPYA ILI KIKUNDI CHAO KIWEZE KUPATA TIJA KUBWA ZAIDI.

CHAKE CHAKE PEMBA

MUFTI MKUU WA OMAN, SHEIKH AHMED BIN HAMED AL-KHALIL, AMEWATAKA WAISLAMU KUITUMIA MISIKITI KWA AJILI YA KUAMRISHANA MAMBO MEMA NA KUENDELEZA UISLAMU, NA WASIZIPE NGUVU KHITILAFU ZAO KWANI HAZITOSAIDIA KUPELEKA MBELE MAENDELEO YA DINI HIYO.

AMEYASEMA HAYO KATIKA KIJIJI CHA MKANJUNI CHAKE CHAKE, WAKATI AKIFUNGUA MSIKITI WA ABUU HAMZA, ULIOJENGWA NA JUMUIYA YA ISTIQAMA KUSINI PEMBA, SAMBAMBA NA KUANGALIA MAENDELEO YA SKULI YA SEKONDARI YA FARAHEDY,INAYOMILIKIWA NA JUMUIYA HIYO.

AMESEMA KUA NI WAJIBU WAO KUWA KITU KIMOJA KATIKA KUIPIGANIA DINI YAO KWA KUIMARISHA MISIKITI NA KUISALIA SAMBAMBA KUITUMIA KWA KUPANGA MAMBO YAO YA DINI ILI AMRI ZA MOLA ZIWEZE KUTEKELEZWA IPASAVYO.

KAZI YA MISIKITI NI KUENDELEZA DINI KWA WAUMINI, KUMUABUDU MWENYEZI MUNGU IPASAVYO, HIVYO NI VYEMA KUJENGA UHUSIANO BAINA YA NYUMBA HIZO TAKATIFU KWA NIA YA KUKUZA UDUGU WA KIISLAMU KWANI LENGO LAO WOTE NI KWA AJILI YA ALLAH.

AIDHA SHEIKH KHALIL AMEWAPONGEZA WALIMU NA WANAFUNZI WA SKULI YA SEKONDARI YA FARAHEDY, YA ISTIQAAMA PEMBA, KWA JUHUDI WALIZOCHUKUA KATIKA SUALA ZIMA LA KUTAFUTA ELIMU, KAZI AMBAYO NI MUHIMU KWAO NA KUSEMA HUKO NDIKO KUFUATA NYAYO ZA MTUME MUHAMAD( SAW).

WILAYA YA MAGHARIBI

WAZAZI NA WALEZI WA WATOTO VISIWANI ZANZIBAR, WAMETAKIWA KUWA NA USHIRIKIANO MZURI BAINA YAO NA WALIMU, KATIKA KUFUATILI ELIMU YA WATOTO WAO, HATUA ITAKAYOSAIDIA KUONGEZA IDADI YA WANAFUNZI WANAUFAULU KATIKA MASOMO

HAYO YAMEELEZWA NA MWALIMU MKUU WA SKULI YA MAUNGANI RAJAB RAMADHANI RAJAB,WAKATI AKIZUNGUMZA NA CHUCHU FM HUKO OFISINI KWAKE MAUNGANI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.

MWALIMU RAJAB AMEWATAKA WAZAZI NA WALEZI WA WANAFUNZI WA SKULI HIYO KUWA NA MASHIRIKIANO NA WALIMU PAMOJA NA KUHUDHURIA VIKAO VYA KAMATI YA SKULI, ILI KUFAHAMU MAMBO MUHIMU JUU YA MAENDELEO YA WATOTO WAO.

AIDHA AMESEMA WAZAZI NA WALEZI NI LAZIMA WAWAZUIE WATOTO WAO KUCHUKUA SIMU SKULI, KWANI WANAPOFIKA MADARASANI HUWA HAWAZINGATII MASOMO WANAYOFUNDISHWA NA BADALA YAKE HUSHUGHULIKIA SIMU ZAO.

KWA UPANDE MWENGINE, MWALIMU MKUU HUYO AMEWATAKA WANAFUNZI WA SKULI HIYO KUFANYA BIDII KATIKA MASOMO WANAYOFUNDISHWA, KWANI ILI WAWEZE KUFAULU MITIHANI YAO YA TAIFA NAN KUJIJENGEA MAZINGIRA MAZURI YA MUSTAKBALI WA MAISHA YA BAADAE

No comments:

Post a Comment