Jul 8, 2011

HAYA NIMAWAZO YANGU KWA KAMPUNI HII

PENDEKEZO LA KUANZA MCHAKATO WA KUBORESHWA KWA MUUNDO ULIOPO SASA WA KITUO CHA REDIO CHUCHU FM, UTAKAO CHUKUA MIEZI MITATU KUTOKA MWEZI WA KUMI MPAKA MWEZI WA KUMI NA MBILI ILI KUWA NA CHUCHU FM MPYA YA MWAKA 2012.
BY MFAUME PASTORY
TAREHE 7-7-2011
SHUKRANI
SINA BUDI KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA JOPO LA UONGOZI WA CHUCHU FM RADIO, KWA USHIRIKIANO MZURI ILIONIPATIA NA INAOENDELEA KUNIPATIA.
SINA BUDI KUWAPONGEZA KWA USIKIVU MLIONAO WAKUZIKUBALI HOJA ZINAZOFIKISHWA MBELE YENU NA KUZIJADILI PASI KUPUUZIWA KWANI HIYO NDIO SIFA KUBWA YA UONGOZI BORA.
NAWASHUKURUNI SANA NA NIWAPONGEZA KWA HILO.
UTANGULIZI
MIMI KAMA MFAUME PASTORY NILIYE KATIKA WAKATI WA MAJARIBIO NDANI YA KAMPUNI HII NINAWASILISHA PENDEKEZO HILI KWENU: PENDEKEZO LA KUANZA MCHAKATO WA KUBORESHWA KWA MUUNDO ULIOPO SASA WA KITUO CHA REDIO CHUCHU FM, UTAKAO CHUKUA MIEZI MITATU KUTOKA MWEZI WA KUMI MPAKA MWEZI WA KUMI NA MBILI ILI KUWA NA CHUCHU FM MPYA YA MWAKA 2012.
CHANZO CHA TATIZO
KWA UPEO WANGU WA KAWAIDA NILIONAO KIFIKRA, KWA MUDA WOTE HUU ADHIMU MLIONIPATIA KUWA NANYI NIMEJIFUNZA MENGI KAMA MWANATAALUMA KATIKA TASNIA HII YA HABARI NILIE NA DHAMIRA YA KULETA MAENDELEO:
HIVYO NAOMBA KUTUMIA NAFASI KUBAINISHA HAYA MAPUNGUFU MACHACHE, AMBAPO NAHAKIKA KUA YAPO BAADHI MNAYOYATAMBUA AMBAYO KWANGU NINAYABAINI KUA YANAWEZA KUA KIKWAZO CHA MAENDELEO YAKAMPUNI HII:
TATIZO LA KWANZA NI: AINA YA UONGOZI/UENDESHAJI WA KAMPUNI
NDUGU VIONGOZI, KAMPUNI YEYOTE INAPOANZISHWA VIONGOZI WAKE HUKAA PAMOJA NA KUAMUA KUCHAGUA NAMNA/AINA YA UONGOZI WA UTAKAO YUMIKA KATIKA KUIONGOZA KAMPUNI HIYO, AMBAPO HAPA HUWA TUNAPATA AINA HIZI TANO ZA UONGOZI WA KAMPUNI:
Ø AUTHIRITY COMPLIENCE MANAGEMENT: (9-1) HII NI ILE AINA YA UONGOZI AMBAO ASILIMIA 90 HUJALI UZALISHAJI, LAKINI ASILIMIA KUMI TU HUJALI MASLAHI YA WATUMISHI WAKE. Ag WAHINDI WAKO HUMU.
Ø COUNTRY CLUB MANAGEMENT: (1-9) HII NI ILE AINA YA UONGOZI AMBAO ASILIMIA KUMI HUJALI UZALISHAJI, LAKINI ASILIMIA 90 HUJALI WAFANYA KAZI.
Ø IMPOVERISHED MANAGEMENT: (1-1) HII NI ILE AINA YA UONGOZI AMBAO ASILIMIA KUMI HUJALI UZALISHAJI NA ASILIMIA KUMI HUJALI WAFANYAKAZI.
Ø MIDLE OF THE ROAD MANAGEMENT: (5-5) HII NI ILE AINA YA UONGOZI AMBAO ASILIMIA HAMSINI HUJALI UZALISHAJI NA ASILIMIA HAMSINI HUJALI WAFANYAKAZI.
Ø TEAM MANAGEMENT: (9-9) HII NI ILE AINA YA UONGOZI AMBAO ASILIMIA 90 HUJALI UZALISHAJI NA ASILIMIA 90 HUJALI WAFANYAKAZI.
JE UONGOZI WA CHUCHU FM UKO KATIKA KUNDI LIPI KATI YA HAYO?
HAYA NI MATOKEO MADOGO TU YAUTAFITI MDOGO NILIUFANYA, ILA SIKUISHIA HAPO:
TATIZO LA PILI NI: VISION
NDUGU VIONGOZI, KWANZA KABISA NAOMBA KUWEKA WAZI KUA KAMPUNI YEYOTE ILE DUNIANI NILAZIMA ITAKUA NA MAKUNDI: AMBAPO KUNDI LA KWANZA NI KUNDI LA WAMILIKI ILA KUNDI LA PILI NI KUNDI LA WATUMISHI.
HIVYO VISION (TASWIRA YENU YA BAADAE) PIA HUGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI HAYO MAWILI. WAMILIKI LAZIMA WATAKUA NA VISION YAO LAKINI PIA KAMPUNI KWA MAANA YA WATUMISHI KWA UJUMLA HUWA WANA VISION YAO ILA VISION YA WAMILIKI HUBAKI KUA SIRI YAO.
NINAAMINI HATA NINYI KAMA WAMILIKI MNATASWIRA YENU LAKINI TASWIRA HIYO INAPASWA KUTOJUMUISHWA NA TASWIRA YA KAMPUNI/WATUMISHI AMBAPO HUO NDIO MSINGI WA MAENDELEO.TASWIRA WA WATUMISHI HUWA WAZI KWA WATUMISHI WOTE.
HIVYO KWA UTAFITI MDOGO NILIOUFANYA NIDHAHIRI KWAMBA WATUMISHI WANAKWENDA LAKINI HAWAJUI NI WAPI WANALIPELEKA JAHAZI HILI LA CHUCHU FM KWA MAANA YAKWAMBA HAWANA TASWIRA AMBAYO WAO WANAIFUATA.
Ø JE WATUMISHI WANA VISION (TASWIRA) WANAYO IFUATA?
TATIZO LA TATU: MISION
NDUGU ZANGU, MISION (MIKAKATI YA UTEKELEZAJI) KAMPUNI YEYOTE ILE ILIYONADHAMIRA YAKUJITENGEZEA FAIDA NA KUBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WAKE NI LAZIMA IWE IMEJIWEKEA MIKAKATI KATIKA UTEKELEZAJI WAKE.(MBINU)
HIZI NI NJIA/KAZI AMBAZO ZINAPASWA KUFUATWA/KUFANYWA ILI KUIFIKIA TASWIRA (VISION) AMBAYO KAMPUNI IMEJIWEKEA.
Ø JE KUNA NJIA AMBAZO ZIPO KAMA KAMPUNI IMEZIBAINISHA NA ZINAFUATWA IPASAVYO ILI KUIFIKIA TASWIRA HIYO YA WAMILIKI NA WATUMISHI WAKE?
KWASABABU NINACHO KISHUHUDIA NI UTENDAJI USIOKUA NA UFANISI NDANI YAKE.
LAKINI PIA NJIA HIZO ZINANAMNA AMBAYO UONGOZI UNAPASWA KUZIHIMIZA ZIFUATWE ILI KUFIKIA MAFANIKIO. (MOTIVATION)
TATIZO LA NNE NI: POLICY
NDUGU ZANGU VIONGOZI, KAMPUNI YEYOTE ILE NI LAZIMA IWE NA SERA ZINAZOTAKIWA KUFUATWA NA WAMILIKI,VIONGOZI PAMOJA NA WATUMISHI WAKE.
LAKINI TUNAPASWA KUFAHAMU YA KWAMBA SERA HIZI, KWA CHOMBO CHA HABARI ZINAGAWANYIKA.
TUNA SERA ZA KAMPUNI NA SERA ZA NAMNA YA UTANGAZAJI WA VIPINDI VYA RADIO (HOUSE STYLE) HII YOTE NIKATIKA KUHAKIKISHA TUNALETA UTAFAUTI BAINA YETU NA WALE WASHINDANI WETU.
Ø JE TUNASERA ZA NAMNA GANI? NA JE ZINAJITOSHELEZA? NAUFUATILIAJI WAKE UKOJE?
TATIZO LA TANO NI: RELATIONSHIP
NAKUMBUSHA KUA, MAHUSIANO MAZURI NIKITU MUHIMU SANA KATIKA MAENDELEO YA KITU CHOCHOTE KILE.
KAMPUNI INAPASWA KUA NA MAHUSIANO MAZURI NA JAMII INAYO IZUNGUKA,MAHUSIANO MAZURI NA KAMPUNI NYENZAKE ZINAZOFANYA BIASHARA YA AINA MOJA LAKINI PIA MAHUSIANO MAZURI NA MAKAMPUNI TOFAUTI NA TAASISI MBALIMBAL, HII YOTE NIKATIKA KUJENGA MWONEKANO BORA WA KAMPUNI.
HII HUSAIDIA KUONDOKANA NA MATATIZO MADOGO MADOGO KAMA YA SEMINA ZA WATUMISHI NA URAHISI KATIKA UPATIKANAJI WA NEW TECHNOLOGY.
Ø JE, MAHUSIANO YENU YAKO NAMNA GANI?
TATIZO LA SITA NI: SOURCE OF INCOME AND RESEARCH
HAKUNA KAMPUNI ULIMWENGUNI AMBAYO IMEANZISHWA KWA LENGO LA KUJIPATIA FAIDA, IKAWA INATEGEMEA CHANZO KIMOJA CHA MAPATO YAKE, MATANGAZO PEKEE BADO HAYOTOSHI KATIKA KUIMARISHA PATO LAKAMPUNI.
HIVYO UBUNIFU MIONGONI MWA UONGOZI NA WATUMISHI NIMUHIMU SANA KATIKA UENDESHAJI WA VYOMBO HIVI VYA HABARI, KUHAKIKISHA KWA USHIRIKIANO VINABUNIWA VITU VITAKAVYO SAIDIA KUONGEZA PATO LA KAMPUNI.
LAKINI PIA CHOMBO HIKI NI CHOMBO KINACHOHITAJI UTAFITI WA MARA KWA MARA JUU YA VIPINDI LAKINI PIA JUU WASIKILIJI WAKE.
Ø JE TUNAWEZA KUELEZA CHUCHU FM IMEANZISHWA MAALUM KWA KUNDI LIPI LA WATU KATIKA JAMII?
Ø JE KWANINI HAKUNA MATANGAZO MENGINE ZAIDI YA YALE YA KAMPUNI ZA SIMU?
TATIZO LA SABA NI: RESPONSIBILITIES AND SPECILISATION
TATIZO KUBWA AMBALO LIMEKUA LIKIRUDISHA NYUMA MAENDELEO YA KITU CHOCHOTE KILE! NI WATU WAKE KUTOKUTAMBUA VYEMA NINI MAJUKUMU NA WAJIBU WAO.
LAINI PIA TATIZO KUBWA AMBALO LIMEKUA LIKIPELEKEA WATU WENGI KATIKA MAENEO MBALIMBALI KUSHINDWA KUFANYA KAZI ZAO KIUFANISI NI KUTOKUWEPO KWA MGAWANYO WA MAJUKU.
AMBAPO HAPA TUNAKUTANA NA MSEMO USEMAO HAKUNA AWEZAE TUMIKIA MABWANA WAWILI KWA WAKATI MMOJA!!NA NDIO SABABU MAKAMPUNI,MASHIRIKA NA HATA TAASISI ZILIZOENDELEA HUZINGATIA ZAIDI MGAWANYO WA MAJUMU ILI KULETA UFANISI.
HIVYO BASI, TAALUMA, UBUNIFU, UWAJIBIKAJI, UZOEFU NA USIKIVU WA MAWAZO NA KUYAFANYIA KAZI!! NI VITU MUHIMU AMBAVYO HUZINGATIWA ZAIDI KATIKA MGAWANYO WA MAJUKU.
HITIMISHO
HILO NDILO PENDEKEZO LANGU!NA KWA KIWANGO KIDOGO CHA ELIMU NILONAYO KINANITUMA KUA HAYO NIMIONGOZI MWA MAJUKUMU YALIYO NDANI YA UWEZO WANGU.
KWA USHIRIKIANO NINAAMINI KUA HAYO NI BAADHI YA MATATIZO, AMBAYO YANAWEZA TATULIWA NA TUKAWA NA CHUCHU FM MPYA KWA MWAKA 2012.
NOTE: KWA UTAFITI MDOGO NILIOUFANYA, BAADHI YA WATUMISHI WANAMAWAZO YAKIMAPINDUZI, LAKINI WAMEJIKATIA TAMAA!! KWANINI!!!NI KAZI YA UONGOZI SASA KUTAFITI.AMBAPO HUO NDIO UONGOZI BORA.
NIVYEMA USHIRIKIANO KUIJENGA:
Ø TEAM MANAGEMENT: (9-9) HII NI ILE AINA YA UONGOZI AMBAO ASILIMIA 90 HUJALI UZALISHAJI NA ASILIMIA 90 HUJALI WAFANYAKAZI.
AHSANTE

No comments:

Post a Comment