Jul 10, 2011

YALIYOJIRI ZANZIBAR

PEMBA

WALIMU, WAZAZI NA WALEZI KISIWANI PEMBA , WAMETAKIWA KUBADILIKA NA KUACHA TABIA YA KUTUMIA BAKORA KATIKA KUWAADHIBU WATOTO NA BADALA YAKE WATUMIE NJIA MBADALA ZILIZOPO AMBAZO ZINAZOWEZA KUMFUNZA NA KUMTIA ADHABU MTOTO ISPOKUWA BAKORA.

WITO HUO UMETOLEWA NA MRATIB WA MARADI WA KUHAMASISHA ADHABU MBADALA MASHULENI, KUTOKA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR , SAFIA ALI RIJALI, WAKATI AKIZUNGUMZA NA MAAFISA ELIMU,WALIMU PAMOJA NA WANAFUNZI KUTOKA SHULE NNE ZA PEMBA.

MRATIB HUYO, AMESEMA KUWA, WALIMU, WAZAZI NA WALEZI WAMEZOEA KUTUMIA BAKORA KATIKA KUWAADHIBU WATOTO JAMBO AMBALO LINALOWEZA KUMFANYA MATOTO KUWA MKAAIDI NA BADALA YAKE SASA WATUMIE ADHABU MBADALA ISPOKUWA BAKORA NA MTOTO ANAWEZA KUFUNDISHIKA.

AIDHA AMESEMA KUWA, BAKORA SIO NJIA NZURI KWA KUREKEBISHA TABIA NA KUWAFANYA WATOTO WAFAHAMU, KWANI ZIPO ADHABU NYINGI ANAZOWEZA KUPATIWA WATOTO, KAMA KUWAPA KAZI NDOGO NDOGO, KUWEKEANA AHADI PALE ATAKAPOFANYA KOSA, KUZUNGUMZA NAO, KWANI BAKORA SIO JAMBO LA KUREKEBISHA TABIA.

MRATIB SAFIA, AMEFAHAMISHA KUWA, LENGO LA MRADI HUO NI KUHAMASISHA WALIMU, WAZAZI NA WALEZI KUACHA KUTUMIA ADHABU YA VIBOKO KWA WATOTO NA BADALA YAKE KUTUMIA ADHABU MBADALA AMBAZO HAZITAWAATHIRI WATOTO KIMWILI, KIAKILI NA KISAIKOLOJIA.

NAYE AFISA MDHAMINI WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI PEMBA, MOH’D IDDI JUMA, AMESEMA KUWA, MATUMIZI YA BAKORA YAMEONEKANA KULETA MADHARA MAKUBWA MASHULENI, IKIWEMO KUSABABISHA ULEMAVU WA VIUNGO KWA BAADHI YA WATOTO.

PIA AMEBAINISHA KUWA, UKOSEFU WA AMANI NA HOFU HUREJESHA NYUMA AMANI NA MAENDELEO YA WANAFUNZI KUTOKANA NA MATUMIZI YA BAKORA, ILI KUWEZA KUONDOSHA HALI HIYO NI KUHAKIKISHA WANANFUNZI WANAPATA ADHABU MBADALA INAYOWAJENGA ZAIDI KITAALUMA NA KUPATA HAKI YAO YA MSINGI ELIMU YA LAZIMA.

 
 
 
 
 
 
 
WILAYA YA KUSINI
 

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 5.5 ZIMEKUSANYWA NA JUMUIA YA MIKOPO NA MAENDELEO YA JOZANI (JOCDO), WILAYA YA KUSINI UNGUJA , IKIWA NI MICHANGO YA WANAVIKUNDI WANACHAMA 437 INAYOJUMUISHA WANACHAMA 11,750.

AKIWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI NA MATUMIZI, KWENYE MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI,AMBAO UMEFANYIKA SKULI YA KITOGANI, NAIBU KATIBU WA JUMUIA HIYO MUSTAFA MAKAME, AMESEMA KUA, KIWANGO HICHO CHA FEDHA KILIKUSANYWA KUANZIA JULAI MWAKA 2007 HADI JUNI 2011.

AMESEMA KUA KATIKA KIPINDI HICHO CHA MIAKA MINE, WANACHAMA WANAWAKE PEKEE WAKIWA NI ELFU TISA MIA MBILI TISINI NA MBILI,WALIKUSANYA KIASI CHA SHILINGI MILION MIA NNE KUNI NA NANE ELFU, LAKI TANO NA ELFU HAMSINI(418, 950, 000),WAKATI KWA UPANDE WA WANAUME WAKIWA NI ELFU MBILI MIANNE HAMSINI NA NANE (2,458), WAMEKUSANYA JUMYA YA HISA MILION HAMSINI NA TATU, LAKI NANE NA TISINI NA MOJA ELFU.(53,891, 000).

KUFUATIA MAKUSANYO HAYO, JUMUIA IMEWEZA KUTOA MIKOPO YENYE THAMANI YA SHILINGI MILION MIANANE ISHIRINI NA SITA,LAKI NANE NA THELATHINI NA NNE ELFU (826,834,000) ,NA WANAWAKE WALIOBAHATIKA WALIKUA NI ELFU SITA MIATISA THELATHINI (6,930), WAKATI WANAUME WALIKUWA ELFU MOJA MIA TATU SABINI NA MOJA(1,371), KUTOKA VIKUNDI MBALI MBALI VYA WILAYA TANO ZA UNGUJA.

MPEMA AKIFUNGUA MKUTANO HUO ULIOAMBATANA NA UCHAGUZI ,MKUU WA WILAYA YA KUSINI HAJI MKUNGU MGONGO, AMEWATAKA VIONGOZI WA VIKUNDI MBALI MBALI, MBAVYO NI WANACHAMA WA JUMUIA HIYO YA JOCDO, KUWAHARAKISHA WANANCHAMA WAO ILI KUREJESHA MIKOPO.

KATIKA UCHAGUZI HUO VIZAA MAKONDE MONDI AMECHAGULIWA KUA KATIBU MKUU, JUMA SULEIMAN KHAMIS MWENYEKITI, NA MAKAMU WAKE SAID DUDE KHATIB PAMOJA NA WAJUMBE SITA WA KAMATI MAALUM YA WANANWAKE.

No comments:

Post a Comment