with Mfaume Pastory
OUR GOVERNMENT IS BETTER TO LOOK THIS
This is another day, i Hope your fine, i want you to look this more indeeply,and i want only to remind and tom have a memory,since we got an indepent is 45 years now,and our goal as a national is to fight against our three enemie ignourant, povert and diseases that we had been told with the father of this nation Mwalimu Julius k Nyerere.
Mwalimu said in order to remove them or to reduce them we can be able to make a good future life of tanzania citizen.
Napotaka tuelekee mimi na wewe leo hii ni katika suala moja tu la Ujinga hasa katika suala zima la Elimu ambako tuliowengi wetu tunaamini kuwa ndio msingi na mkombozi wa mwelekeo bora wa maisha yetu.
Lakini kutokana upeo wangu mdogo tu wakufikiria na kuweza kuyaona mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiendelea kutokea katika jamii zetu kwa kwe hili limekuwa likisumbua kabisa akili yangu na kunifanya nione kuwa tunakokwenda sasa tunazidi kupotea.
Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kupambana na adui Ujinga tangu tulipopata uhuru lakini chakushangaza nikwamba wale tuwaonao sisi kuwa ndio wasomi ambao wangeliweza kuwa mstari wa mbele katika upambanaji lakini ndio wamekuwa mstari wa mbele katika kuongeza tatizo la ujinga katika Taifa hili changa.
Pengine swali lako kubwa litakuwa ni akina nani hao? Naomba nikugusie mfano mzuri tu ambako huko ndio utakakoweza kuyaona yote haya na ndio swala ambalo nintalingumzia kiundani zaidi leo hii.
Taasisi zetu mbalimbali za elimu hapa nchini nikiwa na maana ya vyuo na vyuo vikuu hakika baadhi ya taasisi hizi za elimu zimekuwa ndio chanzo kikubwa cha kuzidi kuzidisha kiwango cha watanzania kuonekana kuwa bado ni wajinga.
Zimekuwa zikijitumbukiza katika kuidanganya serikali yetu eidha kwa maslahi yao bunafsi na watumishi wake na si kwa manufaa ya wanafunzi wala kujali mustakabali mzima katika mwelekeo wa maisha yao.
Utaniuliza swali wamekuwa wakiidanganya vipi serikali? Naomba nikufahamisha wewe mtanzania mwenzangu ambae pengine bado uko gizani!
Taasisi hizi ili ziweze kuwa zimekamilika na kuweza kutoa hudu ya elimu kwa watanzania ni lazima ziwe zimepata kibali kutoka kwa wakaguzi wakuu wa serikali ili kuweza kuepuka taasisi holela.
Na ili ziweze kutoa huduma hiyo ni lazima ziwe zimetimiza masharti na vigezo vyote ambavyo vimewekwa na serikali ili kuwezo kutoa kiwango bora cha elimu kwa watanzania.
Sasa kuna baadhi ya Vyuo hapa hapa nchini ambavyo vimekuwa vikitoa elimu ya taaluma hali yakuwa havijatimiza hata nusu ya vigezo ambavyo vimekuwa vikihitajika kwa mujibu wa sheria.
Pengine utaniuliza inakuweje? Serikali imekuwa ikihitaji kuona kama ambavyo nilivyokueleza hapo juu lakini viongozi hawa wa taasisi hizi wamekuwa wakifanya maandalizi ya muda mfupi kwa kuandaa idara feki napengine hata kulazimika kugushi vitendea kazi na kisha kuwaita wakaguzi wa serikali kwa kuwakagau!
Wakaguzi watapanga na kuwaambia siku watakayo kwenda kwa ajili ya shughuli hiyo ya ukaguzi wakifika watakagua na kuona vigezo vyao vipo na hatimae kukipatia chuo hicho usajili lakini pia na pongezi tele.
Walivyo hawana haya watajidai na kuwaelezea mikakati miingi waliyonayo kumbe wakiwalamba visigo wakaguzi hao na mwisho wasiku wanakuwa wametimiza adhma na malengo walokuwa nayo pasipokujua kuwa wameliangamiza taifa huku ni wapi twaelekea?
Hili limetokea katika chuo kimoja maarufu hapa nchini na wala sina haja ya kukiweka hadharani na chuo hicho mpaka sasa kinaendelea kupeta kwa kula ada nyingi za watanzania masikini na nilipoingia ndani kuona kiwango cha ubora wa elimu kitoacho nilisikitika sana.
Huwezi amini chuo hicho maarufu chenye kuofa kiwango cha dipolama nilikikuta kina madarasa mawili ambayo kimekodisha yakitumiwa na wanafunzi zaidi ya mianne na hata vifaa inasemekana wamekuwa wakilia kila mwaka pasipo mafanio yeyote.
Nikajiuliza masuali mengi sana na katika baadhi ya moja ya jibu nililolipata ni ndio kwamana mapaka sasa tunazalisha wasomi hewa ambao tunawapeleka katika soko la ajira wanashindwa kufanya kazi.
Kwani kumbe huko walikotoka katika hivyo vyuo vyao walishindwa kupata mafunzo yaliyo katika viwango vyenye ubora kwani vyuo hivyo havina uwezo huo hili ni jambo ambalo serikali inapaswa kulitazama.
Sidhani kama serikali itakuwza hilitambui suala hili la hasha! Mnalitambua na kama mlikuwa hamlitambui basi ndio mlitambue sasa kwani watu hawa ndio wanao zidi kudidimiza jitahihada zetu katika suala hili changa.
Sasa hebu tuwaulize ninyi
.
viongozi wa taasisi kama hizi nini dhamira yenu kuyafanya haya? Je madhara yake hamuyaoni kwa hao munaowapotezea muda wao? Au huwa mwajisikiaje pale muwaonapo hao wanafunzi wenu baada ya kupata kazi na kurudi kuwauliza lile ambalo hamkuwapatia pindi walipokuwa katika vyuio vyenu?
Mikopo kila kukicha mabeni yanato tena kwa kuwapatia kipaumbele ninyi wenye mataasisi makubwa mkidhaniwa ndio wenye umuhimu zaidi ako wapi kukopa na kuhakikisha mnatoa elimu iliyo bora?
Serikali, pengine hili linafanywa kwa ushirikiano na baadhi yawatumishi wenu serikalini kwakupatiwa kile wanachoita kitu kidogo na viongozi wa taasisi hizo na hawa nao munapaswa kuwashughulikia kwamujibu wa sheria kwani hatutafika kwa mwenendo huu
No comments:
Post a Comment